Magu ni Wilaya Yetu, Magu ni Kwetu.
Pengine haya siyo mazingira mageni kwako kama ni Mwanamagu. Lakini la msingi sana ni Taswira ya Mji wetu wa Magu. Taswira ya mji wowote hapa nchi kwetu ni mazingira ya safi hasa ya kituo cha mabasi au stand ambapo ndipo wageni wengi hufikia kabla ya kuingia maeneo mengine ya Mji.
Haya ni Mazingira ya Stand Magu |
Pengine haya siyo mazingira mageni kwako kama ni Mwanamagu. Lakini la msingi sana ni Taswira ya Mji wetu wa Magu. Taswira ya mji wowote hapa nchi kwetu ni mazingira ya safi hasa ya kituo cha mabasi au stand ambapo ndipo wageni wengi hufikia kabla ya kuingia maeneo mengine ya Mji.
Hiki ni choo cha Kulipia Magu |
Mazingira ya Nje Choo cha Magu Bus Stand |
Wakati huo huo, katika vituo vingi vya mabasi,
vinauzwa vyakula na vinywaji mbalimbali, kwa maana ya vile vya migahawani na vyakula
vinavyouzwa na wafanyabiashara wadogo wadogo mikononi. Kutokana na fursa hii,
ni dhahiri kuwa wasafiri wengi wanaopita kwenye kituo cha mabasi Magu, ambao
wengi wao ni Watanzania wenzetu, inawalazimu kutumia vyoo ili kukidhi haja
walizokuwa nazo.
Kwa maana hiyo vituo vingi vya mabasi hapa nchini vimejengwa kwa minajili ya kuwa na vyoo ili kuwafanya wasafiri, wasipate taabu pale watakapojisikia kushikwa na haja ya kutembelea vyooni. Kwa mfano ukitembelea baadhi ya Wilaya Tanzania hii, utajionea sehemu nyingi zenye mazingira mazuri na masafi ya vyoo.Wilaya ya Nyamagana, Same, Nzega, Maswa kwa kutaja chache wako juu sana kwenye suala la usafi wa vyoo.
Haya ni Matenki ya Kuhifadhia Maji ambayo hata hivyo hayatoshi |
Katika Wilaya yetu ya Magu, yaani Magu Stand kuna choo kimoja ambacho hali yake ya usafi hairidhishi kabisa. Pamoja na ukweli kwamba wasafiri wengi sana hupitiia kwenye kituo hiki, tatizo linakuja pale abiria au msafiri, anaposhikwa na haja, inabidi aende msalani lakini kwa shingo upande.
Ni haki ya wanamagu, watanzania
na wasafiri wote wanaopita Magu Stand kuwekewa mazingira safi ya choo ikiwemo
kuwepo kwa maji ya kutosha ili kuwafanya wajisikie huru, pindi haja zitakapo
washika wanapokuwa safarini au kwa wale wanaoshinda wakifanya shughuli zao mbalimbali
pale Stand.
Choo cha Magu kinavyoonekana kwa Nje |
Kwa upande mwingine, kwa kuwa
vyoo hivi vimepewa watu binafsi kuviendesha au kusimamia, basi watu hao wana
wajibu wa kuvitunza kwa kuvisafisha kiukweli kabisa ili uchafu unaoonekana
kung’ang’ania kwenye kuta uondoke na kuacha mazingira safi. Ni aibu kuwa mkusanya
pesa pekee badala ya kukusanya sehemu ya pesa hiyo wakati huo ukiwekeza kwenye
usafi wa choo chenyewe.
Hali kadhalika kutokana na
umuhimu huo, halmashauri ya wilaya ya Magu, inastahili kubeba lawama kwa upande
mwingine kutokana na ulegevu wao katika kulisimamia hili.
Maji safi na salama ndilo
tatizo kuu hasa kuhusu upaikanaji wake. Mapendekezo ya watu wa afya ni kuwa ni
lazima kuwe na vyanzo vya kutosha vya maji kwa kuwa maji mengi sana hutumika
kusafirisha vinyesi na mkojo. Kwa hiyo kwa vyovyote vile ni lazima kuwe na
vihifadhio vya maji ya kutosha ili kuwezesha kukusanya maji ya kutosha kwa kazi
hiyo.
Hii ni chema katika choo hicho |
Utupaji wa kinyesi ulio salama
kama kanuni za afya zinavyoelekeza huweza kusaidia kujikinga na maradhi
mbalimbali ya kuambukiza na ya milipuko ambayo husababishwa na vimelea
vinavyosababisha maradhi hayo, vikitokea kwenye kinyesi au mkojo.
Magonjwa hayo ambayo wanamagu,
watanzania na wasafiri wanaweza kuyapata kutokana na hali hiyo ni pamoja na
yale yanayosababishwa na bakteria, kama vile kipindupindu, typhoid, kuhara,
kuhara damu, na mengine.
Pia kuna yanayosababishwa na
virusi kama vile kupooza (Poliomyelitis), yapo pia yanayosababishwa na protozoa
kama Amoeba na mwisho ni yale ya minyoo mbalimbali na kichocho. Hivyo utupaji
wa kinyesi unaofuata kanuni za afya ni wa muhimu sana ili kuwalinda wanamagu
wote hasa wanaotumia vyoo hivyo.
Uchafu wa mazingira kwenye kituo
chetu cha basi cha Magu utatusababishia magonjwa katika jamii, ili kuepuka
uchafuzi wa mazingira kwenye kituo hatuna budi kuzingatia, misingi ya afya
binafsi, usafi wa mazingira na, kuhakikisha uchafu hauzagai ovyo.
Sehemu ya kujisaidia haja ndogo(Mkojo) |
Hii ni sehemu ya kuosha mikono ambayo nayo haina muonekano wa usafi chooni hapo |
Taasisi husika zikishirikiana
na vyombo vya habari vichukue jukumu la kuelimisha wasimamizi na watumiaji
wakubwa wa vyoo hasa pale wilayani ili kuwahamasisha na kushirikiana na jamii
katika masuala ya usafi wa mazingira yote ya Stand Magu.
Ikumbukwe kwamba kinga ni bora
kuliko tiba, hivyo juhudi za makusudi hazina budi kufanywa ili kuondosha kabisa
tatizo hili lenye athari kubwa ki afya na mazingira kwa ujumla. Tukiamua
tunaweza kabisa kufanikisha hili, wala hatuhitaji mjomba toka nje.
“Pamoja Tunajenga Magu yenye
Maendeleo Endelevu”