KATIBA
YA UMOJA WA WANAMAGU 2009
MAGU
DEVELOPMENT INITIATIVE (MDI)
TWIKOMIGE
2009
1. UTANGULIZI
1. MISINGI
YA KATIBA
KWA
KUWA SISI Wana -Magu rasmi na kwa dhati tumeamua kuungana kwa shughuli za
maendeleo ikiwa kama msingi wa kujenga jamii inayozingatia uhuru, haki, udugu
na amani,
NA
KWA KUWA uhamasishaji wa shughuli za kiuchumi, jumuiya na urafiki miongonimwa
wana Magu ni muhinu kwa maendeleo na ambayo inaweza kusaidia jamii kujua sehemu
muhimu za maendeleo,
NA
KWA KUWA Magu ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na watu wake ndiyo nguzo
na
nguvu kazi kuu ya kuleta maendeleo Wilayani humo, na kutowajibika kwao katika
shughuli za maendeleo au kwa mchango wowote ule, ni sawa na kutoliendeleza
taifa zima la Tanzania,
KWA
HIYO BASI, sisi kama wananchi wa Tanzania wazaliwa wa Magu tunaoishi Dar es
salaam tumeamua kuungana na kuunda jumuiya ambayo itafuata katiba hii.
2. TAFSIRI
YA MANENO
Tafsiri
ya maneno katika katiba hii ni kama ilivyoelezwa hapa chini isipokuwa pale
itakaposemwa vinginevyo katika katiba hii:
“Magu”
“Magu”
Wilaya ya Magu ambayo ipo Mkoa wa Mwanza, Tanzania;
“MDI”
“MDI”
Magu Development Initiative (Jumuiya ya Uhamasishaji Maendeleo Magu) Ni kikundi
cha hiari kilichoanzishwa kwa mujibu washeria na kanuni za Mashirika yasiyo ya
kiserikali;
“TWIKOMIGE”
“TWIKOMIGE”
Tuhimizane kuleta maendeleo;
“Katiba”
“Katiba”
Mwongozo
wa kanuni na sheria zinazolinda maslahi ya jumuiya na wanachama;
“Mfilisi”
“Mfilisi”
Taasisi iliyoteuliwa kusimamia mali za mashirika
yanayovunjika au kufilisika;
“Mwanachama”
“Mwanachama”
Mtu
yeyote aliyetimiza masharti na kujiunga na Magu Development Initiatives (MDI);
2. IBARA
1
1. JINA
LA JUMUIYA
Jumuiya
itaitwa “Magu Development Initiative” (MDI/ TWIKOMIGE)
Jumuiya
itakuwa ni ya hiari, isiyotengeneza faida, isiyo ya kiserikali na ambayo
imeanzishwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za Mashirika yasiyo ya kiserikali
2. MAKAO
MAKUU
Makao
Makuu ya asasi yatakuwa ni Dar es salaam Tanzania. Shughuli zote za umoja
zitafanywa kwenye makao makuu ya umoja na sehemu zingine zozote kama
itakavyosemwa katika katiba hii.
3. LUGHA
RASMI
Lugha
zitakazotumika katika umoja zitakuwa ni Kiswahili na Kiingereza
4. DIRA
Kuona
jamii iliyohamasika na inayojishughulisha katika maendeleo ya watu wake,
kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia hali halisi ya mazingira, utamaduni na
teknolojia endelevu.
3. IBARA
2
1. MALENGO
YA JUMLA
Lengo
la jumla la umoja huu litakuwa ni kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya
Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelemisha na kuhamasisha
wananchi kuendeleza utamaduni na tabia ya kufanya kazi kwa ushirikikiano
unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha bora kwa watu
wote katika familia na jamii kwa ujumla ili kujenga amani, umoja, haki, udugu,
demokrasia, elimu, uchumi, utawala bora, na mazingira nadhifu katika jamii.
2. MALENGO
MAHUSUSI
a)
Kufanya
utafiti, kuhamasisha na kubaini changamoto mbalimbali za maendeleo
zinazoikabili Wilaya ya Magu;
b)
Kuhamasisha
jamii kushiriki kikamilifu katika huduma za awali za afya, uzuiaji wa magonjwa
ya kuambukiza hususani UKIMWI, Kifua Kikuu nk;
c)
Kuwaandaa
wanawake na wanaume wote kwa pamoja kukabiliana na maisha ya utandawazi hasa
katika kuhamasisha matumizi ya teknolojia endelevu;
d)
Kuhamasisha
utunzanji wa mazingira hasa hifadhi na utunzanji maliasili (ardhi, uoto wa
ardhi, ziwa, mito, milima nk) ili koboresha mazingira kwa maisha bora;
e)
Kusaidia
na kubuni njia mbadala za kuwasaidia wale wote wasio jiweza hasa maskini, walemavu,
yatima, watoto wa mitaani pamoja na makundi yote yanayohitaji misaada;
f)
Kuhamasisha
na kufanya harambee mbalimbali kwa ajili ya kuboresha miradi ya jumuiya yetu;
g)
Kutoa
elimu, habari mbalimbali kwa wanajumuiya na kuhamasisha ushrikiano;
h)
Kuhamasisha
na kujenga uwezo wa makundi mbalimbali ya wanachama na jamii kuanzisha na
kuendeleza miradi ya maendeleo na uzalishaji;
i)
Kupanua
eneo la kiutendaji ili kuweza kuwafikia wana Magu wengi zaidi ambao
wametawanyika kokote dunia;
j)
Kujenga
mtandao wa ushirikiano na taasisi, makampuni, serikali, wafadhili na watu
binafsi ili kubadilishana ujuzi, uzoefu katika harakati za maendeleo;
k)
Kuhamasisha
na kushirikiana na jamii yote ya Watanzania kupambana na rushwa;
l)
Kuhamasisha
na kuhakikisha usawa wa jinsia katika jamii kulingana na kanuni zinazosimamia
maendeleo katika jamii yetu;
4. IBARA
3
1. UANACHAMA
Jumuiya
yetu itakuwa na aina zifuatazo za wanachama:
a) Kutakuwa
na wanachama waasisi ambao watakuwa ni wale wote watakaokuwepo hadi siku ya
mkutano wa mwisho kabla ya kusajili Umoja wetu. Wanachama hawa pia watatakiwa
kulipa kiingilio kiasi cha shilingi 50,000/= na malipo ya mwezi ni kiasi cha
shilingi 10,000/=.
b) Kutakuwa
na wanachama wa kawaida ambao watakuwa ni Watanzania wote wanaotoka katika
Wilaya ya Magu wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55 ambao watakubaliwa kujiunga
baada ya kulipa kiingilio kiasi cha shilingi 50,000/= na malipo ya mwezi kiasi
cha shilingi 10,000/=.
c) Kutakuwa
na wanachama wa heshima ambao watakuwa ni Watanzania kutoka Magu wenye umri
kuanzia miaka 56 na kuendelea lakini bado wanaunga mkono shughuli zote za
jumuiya yetu na watatakiwa kulipa kiasi cha shilingi 50,000/= kama kiingilio na
10,000/= kama ada ya mwisho wa mwezi.
d) Kutakuwa na wanachama washirika ambao
watakuwa ni jumuiya mbalimbali ambazo zitakuwa zinatumia na kutegemea sera na
kazi mbalimbali za jumuiya yetu na kutoa misaada ya kifedha. Jumiya hizi
zitalipa ada ya kiingiio cha uanachama kiasi cha shilingi 50,000/= na ada ya
mwisho wa mwezi kiasi ch shilingi 10,000/=.
e) Kutakuwa
na wanachama wa umoja ambao watakuwa ni Jumuiya, Taasisi, Klabu pamoja na Asasi
zote za kiraia. Kiingilio ni shilingi 50,000/= na ada ya mwisho wa mwezi ni
shilingi 10.000/=
2. MASHARTI
YA UANACHAMA
Ili mtu awe mwanachama wa MDI ni lazima akidhi
vigezo vifuatavyo:
a)
Awe
na umri kuanzia miaka 18, mwenye kupenda kujihusisha na shughuli za maendeleo;
b)
Awe
na tabia njema na anayekubalika kwa jamii;
c)
Awe
tayari kutumia muda wake na hata raslimali kwa shughuli za Jumuiya pale
inapotakiwa;
d)
Awe
tayari kulipa ada, kiingilio na michango mbalimbali kwa maendeleo ya Jumuiya.
3. TARATIBU
ZA KUOMBA UANACHAMA
a) Kujaza
fomu maalumu ya maombi ambayo itapatikana kwenye ofisi ya Katibu wa TWIKOMIGE.
Majibu yatatolewa baada ya Mkutano Mkuu kujadili maombi ya mwanachama husika;
a) Kulipa
kiingilio cha uanachama kiasi cha shilingi Elfu Hamsini (Tshs50,000/=)
b) Kuwa
tayari kulipa ada ya shilingi Elfu Kumi kwa kila mwezi (Tshs10,000/=)
4. HAKI
ZA MWANACHAMA
Kila
mwanachama ana haki ya:
a) Kuchagua
viongozi na kuomba kuchaguliwa katika uongozi;
b) Kuwa
huru kutoa maoni yake kuhusu uendeshaji wa shughuli za Jumuiya;
c) Kujitetea
kabla ya kuchukuliwa hatua na uongozi/wanachama;
d) Kupata habarí/ taarifa za maendeleo na
mwenendo wa shughuli zote zinazofanywa na Jumuiya kwa njia za uwazi.
5. WAJIBU
WA MWANACHAMA
Kila mwanachama ana wajibu wa:
a) Kuhudhuria
vikao vyote vya Jumuiya kwa mujibu wa Katiba hii;
b) Kushiriki
katika shughuli za Jumuiya kama itakavyoelekezwa na uongozi;
c) Kutumia
na kusimamia kwa uangalifu raslimali za Jumuiya;
d) Kutoa kiingilio na michango mingine
itakayopitishwa na vikao halali vya Jumuiya;
e) Kutunza
siri na taarifa nyeti za Jumuiya;
f) Kutumia
vizuri na kutunza rasilimali za Jumuiya.
.
6. KUKOMA
UANACHAMA
Uanachama
utakoma kwa:
a) Kutokana
na kifo cha mwanachama;
b) Kujiuzulu
kwa hiari;
c) Kutolipa
ada kwa muda wa miezi sita mfululizo;
d) Kutohudhuria vikao vitatu mfululizo
bila taarifa kwa uongozi;
e) Kufukuzwa
kwa uamuzi wa wajumbe wa mkutano mkuu;
f) Mwanchama
yeyote, uanachama wake uliokoma kwa sababu zilizotajwa hapo juu hatarudishiwa
kiingilio na michango yote aliyotoa;
g) Mwanachama
aliyefukuzwa akipenda kujiunga tena atalizimika kufuata masharti kama
yalivyoainishwa katika kifungu hapo juu;
h) Mwanchama
aliyefukuzwa kwa makosa ya ugomvi, wizi au vitendo vyovyote; vinavyoweza
kuaibisha, kuharibu na kutweza jina la Jumuiya, hataruhusiwa kujiunga tena na
Jumuiya TWIKOMIGE.
7. MLEZI
KIUME/ KIKE
Kutakuwa
na mlezi ambaye atatokana na wanachama wa heshima. Huyu atakuwa ni mshauri wa
jumuiya yetu. Mlezi atapendekezwa na Mkutano Mkuu wa Jumuiya na jina lake
kuhakikiwa na Mkutano Mkuu wa mwisho wa Mwaka.
8.
KUKOMA KWA ULEZI
Mwanachama
atakoma kuwa mlezi kama kati ya mambo yafuatayo yatatokea:
a)
Kama
atafariki;
b)
Kama
kutakuwa na udanganyifu wowote katika uptishwaji wa Jina Lake;
c)
Matumizi
mabaya ya madaraka;
d)
Kama
atajiuzulu wadhifa huo baada ya kuandika barua kwa Katibu ya kuomba kufanya
hivyo ndani ya siku 30;
e)
Matatizo
ya kiafya;
f)
Baada
ya kupatikana na hatia mahakamani na kufungwa jela kwa muda unaozidi miezi 6.
5. IBARA
4
1. MATAWI
YA TWIKOMIGE
a)
Jumuiya
inaweza kufungua matawi mbalimbali katika eneo laTanzania pale itakapoonekana
kuwa ni sawa kutegemea na malengo ya umoja wetu;
b)
Tawi
litafunguliwa pale tu ambapo mkutano mkuu utakuwa umeridhia kuanzishwa kwa tawi
hilo na baadae kupitishwa na mkutano wa mwisho wa mwaka;
c)
Kila
tawi litafanya shughuli zake kwa kutumia katiba hii lakini litaruhusiwa kuwa na
kanuni zake mbalimbali ambazo hazitakuwa tofauti na malengo ya katiba hii;
d)
Mkutano
mkuu utakuwa na uwezo wa kusimamisha shughuli za tawi lolote ambalo litakuwa
linafanya shughuli zake kinyume na malengo ya katiba hii;
e)
Hakuna
tawi lolote litakalokuwa nauwezo wa kubadilisha katiba hii au kuwa na katiba
tofauti na katiba hii.
6. IBARA
5
1. VIONGOZI
WA TWIKOMIGE
Kiongozi
ni Mwanchama yeyote atakayepewa dhamana na wanachama kusimamia shughuli za
Jumuiya, ama kwa kuchaguliwa au kuteuliwa na mamlaka husika.
2.
SIFA ZA KIONGOZI
a)
Awe
mwanachama hai (wa jinsia yeyote) mwaminifu na mwadilifu;
b)
Awe
anajua kusoma na kuandika na yupo tayari kujifunza na kujiendeleza;
c)
Mwenye
uwezo wa kubuni na kusimamia shughuli binafsi na za jamii;
d)
Mwenye
uwezo au kipaji cha kuwezesha watu kufanya kazi kwa ushirikiano.
3.
TARATIBU ZA UCHAGUZI WA UONGOZI
a)
Wanachama
wenye nia ya kuwa viongozi wa Jumuiya watatuma maombi ya maandishi kwa nafasi
za uongozi wanazotaka kushindania;.
b)
Viongozi
watachaguliwa kwa kupigiwa kura za siri na wajumbe halali waliohudhuria katika
Mkutano Mkuu;
c)
Uchaguzi
utafanyika tu endapo idadi ya wajumbe wa halali kupiga kura ni nusu ya
wanachama hai;
d)
Endapo
wagombea wa nafasi ya uongozi watapata kura zinazolingana kwa mara ya kwanza,
kura zitarudiwa kupigwa ili kupata mshindi;
e)
Endapo
wagombea wa nafasi ya uongozi watafungana tena katika duru ya Pili ya uchaguzi,
Mwenyekiti atatumia kura ya turufu kuamua ushindi.
4.
SAFU YA VIONGOZI
TWIKOMIGE
itakuwa
na safu ifuatayo ya uongozi:
a) Mwenyekiti;
b) Makamu
mwenyekiti;
c) Katibu;
d) Katibu msaidizi;
e) Mweka
hazina;
f) Mweka
hazina msaidizi.
Viongozi wote
watapatikana kwa njia ya kura ya siri wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwisho wa
Mwaka.
5.
MUDA WA UONGOZI
a) Muda
wa viongozi kukaa madarakani ni miaka miwili mfululizo. Kiongozi anaweza
kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine;
b) Katika
kipindi cha tatu cha uongozi, theluthi moja ya viongozi wa zamani watalazimika
kujiuzulu kutoa nafasi kwa wanachama wengine kushika nafasi za uongozi;
c) Kiongozi
anaweza kuachishwa uongozi endapo atakiuka masharti ya uongozi kulingana na
kanuni zilizokubaliwa.
6.
WAJIBU WA VIONGOZI
i.
Mwenyekiti
a)
Atakuwa
ndiye kiongozi mkuu wa umoja na ataongoza vikao vyote vya jumuiya na atakuwa na
kura ya turufu;
b)
Atakuwa
ndiye msemaji mkuu wa jumuiya;
c)
Atasimamia
na kuhakikisha kuwa kazi zilizopangwa zinatekelezwa na wahusika na kwa muda
muafaka;
d)
Atawakilisha
au atateua mtu wa kuwakilisha Jumuiya katika mikutano na shughuli zingine nje
ya Jumuiya;
e)
Atakuwa
mwanzilishi wa ushirikiano na Jumuiya zingine;
f)
Atakuwa
ni mjumbe wa bodi ya ushauri;
g)
Atakuwa
mmoja wa waidhinishaji malipo na kuweka sahihi katika hati za malipo na hundi.
ii.
Makamu
Mwenyekiti
a)
Atahudhuria
vikao vyote vya jumuiya.
b)
Atafanya
kazi zote zilizo tajwa katika sehemu ya 5.5.1 hapojuu endapo mwenyekiti hayupo.
iii.
Katibu
(a) Ni mtendaji na mratibu wa shughuli za
kila siku za Jumuiya;
(b) Atakuwa mwandishi na mtunza kumbukumbu
na nyaraka zote za Jumuiya;
(c) Ataitisha mikutano yote ya Jumuiya kwa
kushauriana na Mwenyekiti;
(d) Atapokea maombi ya wanachama wapya na
kuyawasilisha kwenye mkutano mkuu;
(e) Atatoa taarifa ya shughuli za jumuiya
katika mkutano mkuu wa wanachama wote;
(f) Atakuwa mmoja wa waidhinishaji malipo
na kuweka sahihi katika hati za malipo na hundi;
(g) Atawajibika kwa Mwenyekiti wa Jumuiya.
iv.
Katibu
msaidizi
Katibu
msaidizi atafanya kazi kama ilivyoainishwa katika sehemuya (c) hapo juu
anapotakiwa kufanya hivyo.
v.
Mweka
Hazina
a) Ni
mtendaji na mratibu wa shughuli za kila siku za Jumuiya;
b) Kupokea
na kutunza fedha za Jumuiya na kutunza vitabu vya fedha;
c) Kutayarisha
taarifa za fedha (mapato na matumizi) na kuisoma katika mkutano wa wanachama
wote;
d) Atakuwa mmoja wa waidhinishaji na mweka
sahihi katika hati za malipo na hundi;
e) Ataratibu
shughuli zote za kuongeza mtaji na kuinua uchumi wa Jumuiya na shughuli za
wanachama;
f) Mshauri
mkuu wa vikundi vya wazalishaji na wajasiriamali.
vi.
Mweka
Hazina msaidizi
Mweka
Hazina msaidizi atafanya kazi kama ilivyoainishwa katikasehemu ya (e) hapo juu
anapotakiwa kufanya hivyo.
7. IBARA
6
1. MIHIMILI
YA JUMUIYA
Kutakuwa na kamati zifuatazo katika jumuiya:
a)
Kamati ya Utendaji;
b)
Mkutano Mkuu;
c)
Sekretariti
d)
Bodi ya Washauri.
i.
Kamati
ya Utendaji
Kutakuwa
na kamati ya utendaji itayoundwa na viongozi wote watano waandamizi wa TWIKOMIGE
pamoja na wajumbe wengine 21 watakaochaguliwa wakati ule ule na kwa
utaratibu ule ule wanavyopatikana viongozi waandamizi wa Jumuiya.
ii.
Kazi
za Kamati ya Utendaji
a) Ni
chombo kitakachohusika kusimamia uendeshaji wa shughuli zote za kila siku za TWIKOMIGE;
b) Ni
muhimili utakaopanga kikao cha mkutano mkuu;
c) Itakuwa
na uwezo wa kutoa nguvu yake kwa kiongozi yeyote wa juu au kamati yeyote ndogo;
d) Itakuwa na uwezo wa kusimamia na
kuhakikisha kuwa utawala wa Jumuiya pamoja na fedha zake ziko katika mazingira
yanayoheshimu Katiba;
e) Itakuwa
na uwezo wa kumusimamisha kiongozi yeyote wa juu wa Jumuiya au mshauri yeyote
baada ya kupata ushahidi wa kutosha unaoonesha matumizi mabaya ya maadili ya
madaraka, ufujaji wa fedha na mengine yanayofanana na hayo kwa kumpigia kura ya
kutokuwa na imani naye na kusubiri maamuzi ya mwisho ya mkutano mkuu;
f) Kamati
ya utendaji kwa madaraka yake au kwa ushauri wa wajumbe, inaweza kuunda nguvu
kazi, kama itahitajika kwa ajili ya utendaji wa majukumu ya dharura kadri
itakavyohitajika;
g) Itakuwa
ndicho chombo cha kutunga será za Jumuiya na itawajibika kwa utawala wa Jumuiya
kwani itashiriki katika kutoa ushauri mbalimbali kwa viongozi ikiwa ni kisheria
kwa wao kutekeleza majukumu yao.
iii.
Mkutano
Mkuu
Kutakuwa
na mkutano mkuu utakaojumuisha wajumbe wote wa kamati ya utendaji,
wawakilishi
kutoka katika matawi yote ya Jumuiya, wanachama waasisi, wanachama wa heshima,
wanachama wa umoja pamoja na marafiki mbalimbali waalikwa. Mkutano utafanyika
tarehe 30 Mei kila mwaka.
iv.
Kazi
za Mkutano Mkuu
a) Ni
muhimili unaochagua viongozi wa Jumuiya pamoja na wajumbe wa kamati ya
utendaji;
b) Utapitia
bajeti ya mwaka ya Jumuiya na utapitisha bajeti ya mwaka unaofuata;
c) Kujadili
na kutoa mapendekezo kwenye ripoti ya Katibu mkuu;
d) Utakuwa na uwezo wa kupitisha au
kukataa majina yaliyopendekezwa kwa ajili ya walezi au washauri. Kufanya kazi
zingine zozote kadri itakavyohitajika na Jumuiya;
e) Itatoa
miongozo na kanuni zote zinazo elekeza mahusiano na matawi mengine ya TWIKOMIGE
na wanachama wote kwa ujumla.
v.
Sekretariati
Kamati
ya utendaji itakuwa na mamlaka ya kuteua sekretariati kwa ajili ya kufanya kazi
za kila siku za Jumuiya kadri itakavyohitajika. Sekretariati itaongozwa na
viongozi wa Kamati ya utendaji ambao watasimamia shughuli zote za Sekretariati
na itakuwa na mamlaka ya kutoa pesa kwa niaba ya Jumuiya nzima hadi kiwango
ambacho kitaelekezwa na kamati ya utendaji.Sekretariati itawajibika kwa Katibu
wa Jumuiya.
vi.
Bodi
ya Washauri
Kutakuwa
na Bodi ya washauri ya Jumuiya, ambayo itaundwa na wajumbe wawili hadi wanane
kutoka nje au ndani ya Jumuiya. Wajumbe wa Bodi ya washauri watapendekezwa na
kamati ya utendaji na watahakikiwa na mkuano wa mwisho wa mwaka. Wajumbe hao wa
bodi ya ushauri watakuwa ni watu wenye tabia njema inayokubalika ndani ya
Jumuiya, wawajibikaji na wako tayari kuindeleza wilaya ya Magu.
vii.
Kazi
za Bodi ya Washauri
a) Itawajibika
kuhakikisha kuwa mali zote na mitaji ya Jumuiya ziko salama.
b) Mali
ya ya Jumuiya, aidha inayohamishika au isiyohamishika itakuwa mikononi mwa Bodi
ya washauri na itakuwa na uwezo wa kushitaki au yenyewe kushitakiwa kwa sababu
itakuwa na uwezo wa kukamilisha mikataba mbalimbali ya Jumuiya.
c) Kwa
mujibu wa Katiba hii, Bodi ya washauri itafanya kazi zake kwa kufuata Katiba
hii pia na sheria zingine zinazohusiana na mambo ya ushauri Tanzania.
viii.
Muda,
Vipindi vya Bodi ya Washauri
a) Wajumbe
wa Bodi ya washauri watashika nafasi zao kwa muda wa miaka miwili (2) na
wataruhusiwa kugombea tena kwa kipindi kingine cha pili;
b) Bodi
ya washauri itakutana mara mbili (2) kwa mwaka.;
c) Bodi
ya washauri watachagua M/Kiti wao kutokana na wajumbe wa Bodi ya wadhamini;
ix.
Kukoma kwa mjumbe kuwa Mshauri:
Mjumbe
atakoma kuwa mshauri endapo mambo yafuatayo yatatokea:
a) Kama
atafariki;
b) Kama
atafanya kazi zake kinyume na utaratibu uliowekwa na Bodi;
c) Kutumia
vibaya madaraka yake;
d) Kujiuzulu wadhifa wake kwa kutoa
maelezo kwa maaandishi ndani ya siku thelethini (30) kwa kamati ya utendaji na
kutoa nakala yake kwa wajumbe wa Bodi ya washauri;
e) Akiwa
na matatizo ya kiafya;
f) Kupatikana
na hatia mahakamani na kufungwa jela kwa muda usiopungua miezi sita (6);
g) Bodi
ya washauri itakuwa na nembo yake yenye maneno “Registrar Advisors of Magu
Development Initiative (MDI)”;
h) Washauri
watalipa faida zote zitakazopatikana kutoka kwenye mali na miradi ya Jumuiya
iliyowekezwa huko kwa Mhazini. Matumizi yoyote ya ziada katika mali hizo kwa
uhakiki uliofanywa na Bodi ya washauri lazima itolewe taarifa yake kwa kamati
ya utendaji ambayo itatoa ruhusa ya matumizi hayo ya fedha;
i) Mshauri
yeyote anaweza kutolewa katika nafasi yake na mkutano mkuu
wa
mwisho wa mwaka kama shughuli zake zitaonekana kuingiza Jumuiya katika
malumbano yasiyoisha. Nafasi zote zinazopatikana zitajazwa kwa utaratibu ule
ule wa kawaida.
8. IBARA
7
1.
VIKAO VYA JUMUIYA
Kutakuwa na vikao vya
jumuiya kama ifuatavyo:
a) Mkutano Mkuu;
b) Mkutano wa Kamati ya
Utendaji;
c) Mkutano wa Dharura.
i.
Mkutano
Mkuu wa mwisho wa Mwaka
(a) Mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka utakuwa
ndicho chombo pekee chenye nguvu ya juu katika Jumuiya kitakachowajibika kwa
sera na kazi za Jumuiya kama ilivyoelezwa kwenye katiba hii;
(b) Utakuwa na mamlaka ya kujibu hoja zote
zilizowasilishwa kwake na mjumbe yeyote wa Jumuiya au kamati ya utendaji kwa
kufuata utaratibu ulioainishwa katika Katiba hii;
(c) Mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka
utafanyika kati ya mwezi Desemba na mwisho mwa mwezi wa pili wa kila mwaka;
(d) Kamati ya utendaji ndicho chombo
kitakachowajibika kupanga agenda za mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka na
kusambaza taarifa miongoni mwa wanachama mwezi mmoja kabla ya kikao ili kupata
maoni pamoja na hoja nyingine mpya kama itakavyohitajika na wajumbe;
(e) Taarifa kikao itasambazwa kwa wajumbe
ndani ya siku 21 katika maandishi kwa wajumbee wote kuwataarifu kuhusu tarehe
rasmi, muda, ukumbi na agenda ya kikao. Mambo yatakayojadiliwa kwenye kikao
yatakuwa ni yale tu ambayo yako katika agenda na si vinginevyo na lazima
yakubalike na wajumbe;
(f) Mwenyekiti wa Jumuiya ndiye
atakayeongoza mkutano mkuu waa mwisho wa mwaka.kama hatakuwepo, makamu
Mwenyekiti atachukua nafasi yake.
Kama
wote hawapo, basi mjumbe mwingine yeyote atachaguliwa kwa muda
ili
kutekeleza majukumu hayo.
ii.
Mkutano
wa kamati ya utendaji
(a) Utakutana
mara moja kila baada ya miezi miwili kama itakavyopangwa;
(b) Utafanya kazi zake zingine kama
ilivyopangwa kwenye katiba hiiI.
iii.
Mkutano
wa Dharura
(a) Mkutano mkuu wa dharura unaweza
kuitishwa wakati wowote katika mwaka mbali na ule ambao umezoeleka mwishoni mwa
mwaka;
(b) Taarifa yake itatolewa siku 14 kabla
kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu;
(c) Mapendekezo ya kuitisha mkutano wa
dharura inabidi yaungwe mkono na angalau theluthi moja ya wajumbe wote wa
mkutano mkuu na yapelekwe kwenye kamati ya utendaji ambayo ndiyo itaitisha
mkutano huo;
(d) Utashughulikia matatizo yote ambayo
yatakuwa yanahitaji utekelezaji wa haraka wa mkutano mkuu.
9. IBARA
8
1.
MWAJIRI WA JUMUIYA
Kamati
ya utendaji ndiyo itakayoshika majukumu yote ya kuajili wafanyakazi au
wataalamu wote wa Jumuiya. Pia wafanyakazi wale ambao wataifanyia kazi Jumuiya
kwa muda fulani; pale ambapo hadidu rejea na masharti ya mwajiliwa yatasainiwa
na pande zote. Waajiliwa wafuatao wataajiliwa na Jumuiya ya TWIKOMIGE:-
a) Afisa
wa programu/ Mkurugenzi;
b) Afisa
wa Utafiti;
c) Watawala
wasaidizi;
d) Watumishi wa muda;
e) Madreva.
10.
IBARA
9
1.
FEDHA
i.
Vyanzo vya fedha
a) Kiingilio
na ada za wanachama;
b) Michango
kutoka kwa miradi ya wanachama inayodhamiwa na TWIKOMIGE;
c) Misaada
kutoka kwa wafadhili, serikali na wa tu binafsi;
d) Mikopo na ruzuku zisizo na riba.
ii.
Usimamizi
a) Jumuiya
itafungua akaunti za fedha katika taasisi za fedha na benki;
b) Fedha
zote zinazokusanywa zitahifadhiwa benki kulingana na kanuni za fedha zilizopo
c) Matumizi
yote ya fedha lazima yaidhinishwe na mamlaka zilizokubalika katika kanuni za
fedha na kutolewa stakabadhi husika;
d) Taarifa za fedha zitatolewa kila baada
ya miezi mitatu (3);
e) Mwaka
wa fedha utaanzia Januari 1 hadi Deseaba 31 ya mwaka husika;
f) Mkutano
mkuu utahakikisha kuwa vitabu vya fedha za jumuiya vimekaguliwa na wakaguzi wa
ndani na nje wenye sifa zinazokubalika.
11.
IBARA
10
1.
AKIDI
(a) Akidi ya vikao vyote vya Jumuiya katika
mihimili yote itakuwa ni mahudhurio ya walio wengi kutegemea na idadi ya
wajumbe katika muhimili husika;
(b) Kila mjumbe katika kila muhimili
atakuwa na kura moja;
(c) Katika vikao vyote vya Jumuiya
Mwenyekiti ndiye kiongozi mkuu, asipokuwepo basi Makamu mwenyekiti atakaimu
nafasi yake. Kama wote awapo, mjumbe yeyote atateuliwa kushika nafasi hiyo kwa
muda;
(d) Mwenyekiti kwa kutumia madaraka yake
aliyopewa na katiba hii anaweza kusitisha michango zaidi kutoka upande wowote
katika hoja yoyote iliyopo mezani;
(e) Wakati wa uchaguzi kura zote zitakuwa
za siri.
12.
IBARA
11
1.
MAAMUZI
Maamuzi
yote yatafanywa katika kikao kwa kufuata maamuzi ya wengi waliohudhuria katika
kikao.
13.
IBARA 12
1.
MAREKEBISHO YA KATIBA
a) Katiba
hii inaweza kufanyiwa marekebisho makubwa au kwa baadhi ya vipengele na mkutano
mkuu;
b) Mapendekezo
ya azimio la kurekebisha katiba ni lazima yaungwe mkono na zaidi ya asilimia
hamsini ya wajumbe waliohudhuria mkutano mkuu;
c) Marekebisho
ya katiba yatawasilishwa kwa msajili wa Jumuiya za kiraia katika muda wa mwezi
mmoja baada ya kupitishwa na wanachama.
14.
IBARA
13
1. NEMBO
YA JUMUIYA
Nembo
ya Jumuiya yetu itakuwa na maneno yafuatayo; “MAGU DEVELOPMENT INITIATIVE”
(MDI) na itatumika katika makubaliano mbalimbali wakiwepo viongozi wawili
na mshauri.
15.
IBARA
14
1. UKAGUZI
WA AKAUNTI
Akaunti
na makablasha yote yatakaguliwa wakati wanachama kumi (10) walioteuliwa rasmi
kwa kazi hiyo wakishuhudia katika makao makuu ya Jumuiya na taarifa itatolewa
ndani ya siku saba.
16.
IBARA
15
I.
KUVUNJIKA
KWA JUMUIYA
a) TWIKOMIGE
inatarajiwa
kufanya kazi zake kwa muda wote kulingana na mahitaji ya wanachama wake. Hata
hivyo, TWIKOMIGE inaweza kuvunjwa endapo litapitishwa azimo la kuivunja
ambalo litaungwa mkono na wajumbe halali wasiopungua theluthi mbili (2/3) ya
waliohudhuria na kupiga kura katika Mkutano Mkuu;
b) Kama
akidi ya kuivunja TWIKOMIGE itakuwa haijafikiwa, pendekezo la kuivunja
TWIKOMIGE litapelekwa katika mkutano mwingine utakaofuata;
c) Akidi
ya mkutano huu itakuwa ni 2/3 ya wajumbe;
d) Hata hivyo pendekezo la kuivunja
TWIKOMIGE litakamilika tu pale ambapo baada ya kupigiwa kura na wajumbe walio
wengi litasainiwa na viongozi watatu waandamizi yaani Mwenyekiti, Katibu na
Mhazini, na baadae kupelekwa kwa msajili wa vyama vya kiraia;
e) Kama
msajili atasaini pendekezo hilo, hakutakuwa na hatua zingine za ziada za
kuchukua, isipokuwa ni kuivunja TWIKOMIGE moja kwa moja;
f) Endapo
TWIKOMIGE itavunjika, raslimali zake zitatolewa kwa Jumuiya nyingine
inayofanya kazi zinazoendana na ndoto na malengo ya TWIKOMIGE;
g) Bodi
ya washauri, kwa kushirikiana na “Mfilisi” anayetambulika itahakiki mali za
Jumuiya na kuwakilisha pendekezo la kukabidhi raslimali kwa wajumbe wa mkutano
mkuu wa mwisho wa mwaka.
No comments:
Post a Comment