![]() |
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu, Bi Naomi Nnko akifafanua jambo wakati wa kikao cha kazi cha viongozi wa shule za msingi Wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacquiline Liana |
Mkurugenzi Mtendaji
wa Wilaya ya Magu Naomi Nnko, amemwagiza Ofisa Elimu wa shule za msingi Yesse
Kanyuma kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wa shule kumi ambazo zilifanya
vibaya katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2012.
Nnko ambaye ni
mwalimu kitaaluma alitoa agizo hilo wakati akifunguakikao cha utekelezaji wa
kazi kwa walimu wakuu, walimu wakuu wasaidizi, waratibu wa elimu kata na
viongozi wa elimu wilayakatika ukumbi wa CCM wilayani Magu.
“Nakuagiza Ofisa
Elimu, kuwachukulia hatua walimu wakuu ambao shule zao zilifanya vibaya katika
matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi na kunipa hatua uliyochukua” alisisitiza.
Aidha Mkurugenzi huyo
alimwagiza ofisa Elimu huyo kuwaandikia barua za pongezi walimu wa shule za
msingi 12 ambao shule zao zimefanya vizuri katika matokeo hayo ya kuhitimu
elimu ya msingi.
Nnko alizitaja shule
ambazo zilifanya vibaya kuwa ni pamoja na Mizwale, Malangala, Chabula,
mwamachibya, Bunyanyembe, Milambi, Bugando, Misungwi, ijinga na Ng’haya.
Aidha aliwapongeza
walimu wa shule 12 ambazo zilifanya vizuri ambapo alizitaja kuwa ni Isandula,
Mahaha, itongo, Magu, Mwalinha, Ng’watelesha, Sesele, Ilungu, igombe, Busami, Makamba
na Masangani.
Kuhusu shule ambazo
hazikufanya vizuri, Mkurugenzi huyo ameagiza idara ya elimu wilayani humo
kufanya uchunguzi wa kina juu ya shule hizo, ambapo pia amempa Ofisa Elimu wa
shule za msingi muda wa wiki mbili awe amewachukulia hatua wakuu wa shule hizo.
Hatua mojwapo
aliyopendekeza kuwachukulia walimu wakuu wa shule hizo ni pamoja na kuwavua
madaraka ya ualimu ukuu, na nafasi zao kuchukuliwa na walimu wengine wenye sifa
nzuri kiutendaji kazi.
Wakati huohuo Mkurugenzi huyo ambaye ni mwalimu
kitaaluma, alikemea
No comments:
Post a Comment