MAGU

Wilaya ya Magu ni moja ya wilaya SABA (7) katika Mkoa wa Mwanza nchini Tanzania, Afrika ya Mashariki. Makao makuu ya wil...aya hii yapo Magu mjini karibu na Mto Simiyu.

Kwa upande wa Kaskazini,inapakana na Ziwa Viktoria,Kusini inapakana na Wilaya za Kwimba, Misungwi na Mkoa wa Simiyu. Upande wa Magharibi inapakana na Jiji la Mwanza na Mashariki inapakana na Mkoa wa Simiyu.

Wilaya ya Magu inaundwa na Tarafa NNE (4) ambazo ni Itumbili, Kahangara, Ndagaru na Sanjo. Tarafa hizi zinaundwa na Kata mbalimbali kama ilivyooneshwa kwenye Jedwali hapa chini;

TARAFA NA KATA ZA WILAYA MAGU

 ITUMBILI
  • Magu Mjini
  • Lubugu
  • Mwamabanza
  • Nyigogo
  • Sukuma 
 KAHANGARA
  • Kahangara
  • Mwamanga
  • Kitongo Sima
  • Nyanguge
 NDAGARU
  •  Ng"haya
  • Shishani
  • Jinjimili
  • Nkungulu
  SANJO
  • Kisesa
  • Bukandwe
  • Bujashi
  • Kongolo
  •  Lutale



No comments:

Post a Comment