Wanamagu Wenzangu natumaini
tunaendelea vizuri na ujenzi wa Taifa nje na ndani ya mipaka ya Tanzania.
Tukiwa tunaelekea kuzuri katika
harati zetu za kupeleka maendeleo wilayani kwetu nimeona leo itakuwa vizuri
kama tukishauriana yafuatayo;
1. Hapo
ulipo ni lazima ujione kuwa ni Kiongozi uliyekamilika, unayetegemewa na ambaye
unaweza kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo pale unapohitajika. Kufanya
hivyo inakusaidia kujiona una nguvu ya kutosha na iliyokamilika na kuondoa
unyonge wote katika viungo vyako.
2. Tunatatakiwa
tuwe wabunifu wa hali ya juu. Ubunifu wetu utatusaidia sana kujiamini na
kujiona kuwa tunaweza kufanya mambo mengi kwa vitendo na sio kwa kujadili
pekee. Tunahitajika kuwa wabunifu wa kubuni miradi na vyanzo vya mapato kwa
ajili ya umoja wetu na ndugu zetu hasa wanaohitaji msaada wetu. Kwa mfano
kutafuta wafadhili na kadhalika.
3. Wakati
mwingine tunaweza kuongeza maarifa kwa kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa. Tanzania
tuna jumla ya wilaya 135, ambazo zipo katika hatua mbalimbali za maendeleo.
Basi tujifunze kutoka huko na tupeleke nyumbani. Wahenga walisema “Kila mbwa
hubwekea mlangoni kwao”
No comments:
Post a Comment