Wednesday, March 20, 2013

Lwakatale afutiwa mashtaka,akamatwa tena

MTUHUMIWA wa kesi ya ugaidi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Chadema Wilfred Lwakatale amefutiwa mashtaka yanayomkabili na kukamatwa tena,kisha akafungulia mashtaka upya.
Kufutwa kwa mashtaka ya Lwakatale inatokana na makosa yaliyofanywa na upande wa serikali, na kumfanya DPP kufuta mashtaka hayo.
Baada ya kuwasilishwa kwa hati hiyo ya DPP, Hakimu Mchauru alikubaliana nayo na kuwafutia mashtaka washtakiwa hao waliokuwa wanakabiliwa na kesi namba 37 ya mwaka 2013, iliyokuwa na mashtaka manne.
Mashtaka hayo ni pamoja na  kula njama ya kutenda kosa la kutaka kumdhuru Dennis Msacky kwa sumu, kushiriki kupanga njama za utekaji nyara, kushiriki katika mkutano wa kupanga kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara na kuhamasisha vitendo vya ugaidi.
Washtakiwa hao wa kesi ya ugaidi walisomewa mashtaka hayo na kurudishwa lumande mpaka April 3 mwaka huu kesi hiyo itakapo somwa tena mahakamani hapo,hata hivyo washtakiwa hao walinyimwa dhama na kutokuruhusiwa kusungumza chochote kwakuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za ugaidi.

No comments:

Post a Comment