Monday, March 18, 2013

Majambazi yapora gari, milioni 200/-*Wachina wanne wajeruhiwa,msako mkali waanza *TANROADS YADAI FEDHA ZILIZOPORWA NI MIL.7.9


MAJAMBAZI 10 wakiwa na bunduki tatu pamoja na mapanga, wamevamia kambi ya Mkandarasi wa Kampuni ya SIETCO kutoka nchini China, iliyopo eneo la Igingilanyi, mkoani Iringa na kupora fedha taslimu sh. milioni 100, dola za Marekani 11,560, euro 54,910 na kuwajeruhi wachina wanne kwa mapanga.

Pia majambazi hao walichukua fedha za Kichina RMB 1,600, kompyuta ndogo 13 (Laptop), kamera mbili za video, simu 12
za mkononi pamoja na gari lenye namba T 693 BVV aina
ya Toyota Pickup.

Uvamizi huo umetokea Machi 15 mwaka huu, saa saba usiku ambapo jana, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ikiongozwa
na Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Christina Ishengoma, ilikwenda eneo
la tukio ili kutoa pole kwa wachina hao.

Akizungumza tukio hilo mbelea ya kamati hiyo, Msemaji kutoka Ubalozi wa China nchini uliopo Dar ers Salaam, Bw. You Jin, alisema SIETCO inataka kusitisha mkataba wa ujenzi kutokana
na usalama wao kuwa mashakani.

 

“Tayari taarifa za kusitisha mkataba zimetolewa katika ofisi zetu  za ubalozi Dar es Salaam, hawa majambazi walitumia mapanga kuwajeruhi wafanyakazi katika vyumba vyao na kuwataka watoe
fedha na kila kitu walichonacho ili wasiwaue kwa risasi,” alisema.

Alisema kamera zilizoibwa zina thamani ya sh. milioni 22,500,000 ambapo wachina waliojeruhiwa ni Lil Chen Yong, Chen Xin Hunk
na wengine aliwataja kwa jina moja moja la Bw, Chui na Bw. Peng.

Aliongeza kuwa, wachina hao wanaendelea kupatiwa matibabu katika zahabati iliyopo ndani ya kambi hiyo chini ya daktari wao
ambaye wamekuja naye kutoka China.

Meneja wa Mradi wa kam puni hiyo ambaye ndie anayesimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Iringa kwenda mkoani Dodoma, Bw. Bai Xuebin, tangu siku ya tukio hadi leo, kampuni hiyo imesitisha shughuli zake.

“Kimsingi usalama wetu uko mashakani ndio maaana tumesitisha shughuli za ujenzi...tunaiomba Serikali iangalie upya suala la umiliki wa silaha kwa watu binafsi ambao baadhi yao wanazitumia kwa kufanya uhalifu kwa kampuni za kigeni ambazi zimekuja nchini
kufanya kazi za maendeleo,” alisema Bw. Xuebin.

Kwa upande wake, Dkt. Ishengoma alisikitishwa na uvamizi uliofanywa na majambazi hao kwa wafanyakazi wa kampuni
hiyo ambao wapo mkoani humo kwa shughuli za maendeleo
ya ujenzi wa miundombinu ya barabara.

“Nauomba uongozi wa kampuni hii pamoja na wafanyakazi, msisitishe shughuli zenu kwani Serikali itahakikisha wahusika
wa uhalifu huu wanafuatiliwa, kukamatwa na kufikishwa
katika vyombo vya sheria,” alisema.

Aliongeza kuwa, Serikali itaongeza ulinzi katika kambi hiyo na kumtaka Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, SSP Nyigesa Wankyo, kuhakikisha ulinzi unaimarishwa eneo hilo.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Iringa, Bw. Paulo Lyakurwa, alisema
fedha taslimu za Tanzania zilizoporwa si sh. milioni 100 kama
ilivyodaiwa na wachina hao bali ni sh. milioni 7,490,000.

Alisema kampuni hiyo inapaswa kuangalia upya juu ya ajira wanazotoa katika shughuli wanayoifanya kwa kuhakikisha
wanaajiri zaidi wenyeji ili kuimarisha usalama zaidi.

“Haya matatizo ya kuvamiwa na kujeruhiwa kama mngekuwa mmeajiri baadhi ya wafanyakazi ambao ni wenyeji, wakati mnapiga kelele za kuomba msaada pengine mngeweza kuupata.

“Kampuni yenu imeshindwa kuajiri wenyeji wanaolizunguka
eneo la kambi ndio maana mlipovamiwa walishindwa kuja ili
kutoa msaada, kuweni na uhusiano mzuri na wazawa,” alisema

No comments:

Post a Comment