Mwanza.
Kutokana na kuenea kwa Dola Bandia za kimarekani katika maeneo
mbalimbali nchini, Polisi MKoani Mwanza inawashilikilia raia wawili wa
Burundi kwa tuhuma za kumiliki noti bandia za marekani 1100 zenye
thamani ya pesa za kitanzania shilingi Milioni moja laki saba na
themanini na mbili elfu.
Kukamatwa kwa raia hao wa Burundi kunafuatia polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanamashaka nao.
![]() | |
Kamanda Mangu |
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ernest
Mangu alisema raia hao wa Burundi walikamatwa maeneo ya uwanja wa ndege
wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 684 ACR.
Kuhusu gari hilo kumilikiwa na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema, Kamanda Mangu, taarifa hizo wanazifanyia kazi, japo
kuwa uhalifu hauna chama
Kamanda Mangu alitoa hadhari kwa wafanyabiashara mkoani Mwanza kutokana na dola bandia za marekani kuzagaa
Polisi inawatafuta watu wengine wakihusishwa kushirikiana na raia hao wa Burundi kutekeleza uhalifu.
No comments:
Post a Comment