![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiriakiano wa Kimataifa Bernard Membe akifafanua jambo |
TANZANIA iko hatarini kuingia katika mgogoro mkubwa wakidiplomasia dhidi ya
nchi za Falme za Kiarabu (UAE) na Saudi Arabia kutokana na tuhuma za kigaidi
zinazo wakabili raia wa nchi hizo.
Taarifa zilizonaswa na MDI Blog kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje ya nchini na Ushirikiano wa Kimataifa zinaeleza kwamba nchini hizo zimeanza
kuihoji serikali uhalali wa kuwashirikilia raia wake.
Hatua ya kukamatwa kwa raia wa nchi hizo kwa tuhuma za ugaidi uliofanyika
jijini Arusha katika Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti nje kidogo ya Jiji hilo
ulioua watu watatu na kusababisha watu zaidi ya 62 kujeruhiwa viabaya ni ishara
mbaya kwa mahusiano ya kidiplomasia.
"Serikali imepokea taarifa kutoka nchi hizo ikihoji uhalli wa raia wake
kukamatwa kwa tuhuma za ugaini, hatua hii inaweza kuwa mbaya zaidi endapo
itabainika kwamba watuhumiwa hao si magaidi, kwani masuala ya diplomasia baina
ya Tanzania na nchi hizo inaweza kuwa mbaya zaidi, tena ukizingatia kwamba
serikali inapata misaada mingi kutoka nchi hizo,kutokana na mahusiano mazuri
baina yetu na wao"kilisema chanzo hicho.
Taarifa hizo pia zilidhibishwa na Waziri Bernard Membe wakati akizungumza na
gazeti moja la kila siku nchini Tanzania ambaye leo anakwenda jijini Arusha
kufuatilia suala hilo na hasa kwa kukamatwa raia wa kigeni wakihusishwa na
tukio hilo, wakiwa ni miongoni mwa watu 12 wanaoshikiliwa na polisi
wakituhumiwa kuhusika na shambulio hilo lililoua watu watatu na wengine zaidi
ya 60 kujeruhiwa.
“Ninakwenda Arusha leo ili kufahamu undani wa suala hili. Baada ya kwenda
ndiyo nitakuwa katika nafasi ya kuongelea mambo haya,” alisema Membe wakati
alipoulizwa jana kuhusu malalamiko ya nchi za Saudi Arabia na Falme za Kiarabu
(UAE) kuhusu kukamatwa kwa raia wao. Watu wanaoshikiliwa na polisi kwa
tuhuma hizi ni pamoja nja Victor Ambrose Calist (20), Mwendasha Bodaboda na
mkazi wa Kwa Mrombo, Jeseph Yusuph Lomayani (18) mwendesha Bodaboda, Mkazi wa
Kwa Mrombo jijini Arusha.
Wegine ni George Batholomeo Silayo (23), mfanyabiashara na mkazi wa Olasiti,
Arusha, Mohamed Sulemani Said (38) mkazi wa Ilala, Dar es Salaam na Jassini
Mbaraka (29) mkazi wa Arusha. Wale wanaotuhumiwa kutoka nje ya Tanzania ni
pamoja na raia wa Falme za Kiarabu (UAE), Said Abdalla Said (28), Abdulaziz
Mubarak (30) na Said Mohsen wakati Jassini Mbaraka (29) anatokea Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment