Moja ya madarasa wanayotumia wanafunzi wa shule ya msingi lupemba iliyoko wilayani magu |
NA Shushu
Joel,Magu
TUMEZOEA
kusikia shule zilizoko vijijini ndani ndani ndizo zinakabiliwa na tatizo la
madawati na majengo,lakini kumbe hata zile za karibu na mijini bado ni shida
kwani shule ya msingi Lupemba iliyoko wilayani magu mkoani mwanza inakabiliwa
na matatizo hayo
Shule hiyo
iliyoko karibu kabisha na ofisi za mji mdogo wa halmashauri ya
magu,inapungukiwa madawati zaidi ya 400 na majengo ya madarasa yasiyopungua 5,
licha ya kuwa karibu na ofisi hizo, lakini cha kushangaza zaidi hakuna kiongozi
wa aina yeyote ile ambaye amefikilia chochote kile juu ya kutatua tatizo hilo
linalowakabili wanafunzi hao wanaosomea kwenye mahema na matofali.
Lupemba shule ya msingi iliyoko wilayani magu wakipata masomo |
Shule hii ya
Lupemba ilifunguliwa rasmi miaka michache tu iliyopita,pamoja na upungufu wa
madawati na majengo bado pia inakumbwa na tatizo la upungufu wa walimu kwani
waliopo ni walimu 8 tu wanawake ni 5 na 3 ni wanaume huku shule ikiwa na jumla
ya wanafunzi 620.
Hayo ni
baadhi tu ya matatizo yanayoikabili shule hiyo ya msingi Lupemba ambayo idadi
kubwa ya wanafunzi wanaishia kukaa chini na kusomea kwenye mahema na huku
wakiendelea na shughuli zao zingine za darasani kama ilivyozoeleka kwa
wanafunzi wetu.
Mwalimu mkuu
wa shule hiyo Daniel Matemi anathibitisha uwepo wa tatizo hilo katika shule
yake na kusema kuwa suala hili hata yeye amelikuta katika shule hiyo ingawa
amekwisha lifikisha katika sehemu husika ila mpaka sasa bado hakuna lolote
lililofanyika.
Shule ya Msingi Lupemba Wilayani Magu Inasikitisha |
“Tumewabana
sana wazazi wa wanafunzi wetu katika michango mbalimbali japo tuweze kuinusuru
shule hii lakini suala hili linakuwa ngumu kwa upande wa wazazi hao nah ii ni
kutokana na siasa chafu zilizopo katika kijiji hiki na hili ni kutofautiana kwa
vyama kati ya mwenyekiti wa shule na mwenyekiti wa kijiji ndio changamoto kubwa
inayochangia kuwaumiza wanafunzi hao.
Mkuu huyo
aliongeza kuwa kilichobaki kwa sasa ni kuwaomba wafadhili walio na moyo ili
wajitokeze kuweza kuifadhili shule hii na kuweza kuinusuru katika janga hili
kwani kipindi hiki cha mvua sijui itakuwaje kwa wale wa darasa la 5,6 na 3
ambao wanasomea kwenye mahema,kwa kusema ukweli watoto hawa wanapata taabu
sana.
“Ndugu
mwandishi kama unavyojua sisi wenyewe hatuna cha kuwasaidia,kama unavyofahamu
kuwa mwanafunzi anayekaa chini unamkosesha mambo mengi sana” alisema mkuu huyo
wa shule.
Lupemba shule ya msingi iliyoko wilayani magu wakipata masomo |
Kwa ujumla
hali hii inawafanya wanafunzi hao kupunguza uwezo wao wa kufanya vizuri
darasani.
Kwa upande
wake Afisa Elimu Msingi wilaya ya magu Yesse Kanyuma alipohojiwa juu ya shule
hiyo alisema kuwa yeye si msemaje juu ya hilo na wala ajui lolote kuhusu shule
hiyo ya lupemba.
N kwa upande
wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Ntinika Paul alipopigiwa simu yake ili kuthibitisha
kwa habari ya shule hii simu yake iliiita bila kupokelewa.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Lupemba Wakiwa Darasani Wakiendelea na Masomo yao Wilayani Magu Mkoani Mwanza |
MWISHO
No comments:
Post a Comment