Monday, March 11, 2013

TAARIFA YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUSOMESHA VIIJANA WENYE UWEZO KIMASOMO SHULENI WANAOTOKA KATIKA FAMILIA ZISIZO NA UWEZO



UTANGULIZI


Umoja wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa kutengeneza faida, wenye malengo ya jumla ya kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelimisha na Kuhamasisha wananchi kuendeleza Utamaduni na Tabia ya kufanya Kazi kwa ushirikikiano unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha bora kwa watu wote katika familia na jamii kwa ujumla ili kujenga Amani,Umoja, Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi, Utawala Bora, na Mazingira Nadhifu katika Jamii.
 
Wanafunzi wenye uhitaji wa kusomeshwa kutoka shule ya Sekondari Itumbili. Kutoka kushoto ni Anastazia Costantine, Samuel Wanga na Emanuel Wilson Maningu walipokutana na wanakamai wa MDI










Hapa wanakamati wetu wakiwa wamefika katoka shule ya Sekondari Itumbili na kukutana na Mwalimu Seif ambaye alikuwa anakaimu Madaraka ya Mwalimu Mkuu wa shule. Kushoto kabisa ni Dr Frank Mganga na Kulia kabisa ni King Sele



WALENGWA
Walengwa wakubwa wa mpango huu ni wanafunzi watatu (3) wa sekondari za kawaida (O-level) wenye uwezo kimasomo darasani lakini wanaotoka katika familia zisizo na uwezo (Maskini)

 
UTEUZI WA WAJUMBE
Jumla ya wajumbe wawili (2) waliteuliwa kutafuta wanafunzi watatu (3) wa sekondari za kawaida (O-Level)wenye uhitaji wa kusomeshwa ambao wanatoka katika familia zisizo na uwezo lakini wenye uwezo shuleni ili wasomeshwe na wajumbe wa MDI. Wajumbe hao ni King Sele na Dr. Frank H. Mganga.



Hapa ni wakati mazungumzo yakiendelea kati ya wanakati King Sele Kulia na Dr. Frank katikati na mwanafunzi Samueli Wanga



Wanakamai na mwanafunzi wakiendelea na mazungumzo zaidi

Dr Frank na King Sele wakichukua Taarifa za Mwanzafunzi Wanga




Mwanafunzi Anastazia Costantine

Mwanafunzi Emanuel Wilson Maningu


UTEKELEZAJI
Wajumbe walianza kazi yao kwa kuzitembelea shule za sekondari za Magu Sekondari na Itumbili sekondari ambapo walibaini idadi ya wanafunzi sita (6) ambao walionekana kuwa na uhitaji kwa kukizi vigezo vilivyokuwa vimewekwa na wadau wa MDI. Kamati hii ilifika tena shule ya sekondari ya Magu tarehe 18/01/2013 nakukutana na wanafunzi hao, viongozi mbali mbali wakiwemo walimu wa shule hiyo na mlezi wa vijana katika shule hiyo. Tarehe 18/02/2013 kamati ilifika shule ya Sekondari Itumbili na kukutana na wanafunzi wenye uhitaji.

Mwanakamati King Sele


Mwanakamati Dr Frank H Mganga


King Sele


Dr. Frank H Mganga

Mwanafunzi Samwel Wanga


Mwanafunzi Samuel Wanga


Dr Frank Mganga




Dr Frank akiwa na Kaimu Mkuu wa shule ya Sekondary Itumbili

Wanakamati waliteta jambo na Kaimu Mkuu wa Shule ya Itumbili




HITIMISHO
Kama ilivyooneshwa hapo juu, zoezi la upatikanaji wa wanafunzi hao linaendelea vizuri na wanafunzi wanatarajiwaa kuwa wamepatikana mpaka mwisho wa mwezi Machi.

 

 










Magu Council won’t apply for change of land use – official

The Magu District Council will not be applying to the government to change Sayaka Game Reserve into a residential area, in Busega and Magu districts in Mwanza and Simiyu Regions, claiming that the Ministry turned down such an application in 2001.

 

The Magu District Council Executive Director, Ms Naomi Nnko, told the ‘MDI’ in Magu recently that her predecessor did the same in 2001 but the Ministry of Natural Resource and Tourism rejected the proposal. “Already, the Ministry of Natural Resource and Tourism has taken a stance on the issue of changing Sayaka Game Reserve to residential area, for people of Magu and Busega in Simiyu and Mwanza regions,” said Ms Nnko.

She was responding to Magu District ward councillors who wanted her to write a letter to the ministry seeking change of use of the reserve to avoid conflicts between the government and residents. She said that the ministry, in a letter dated December 19, 2001, rejected such application and she has failed to file another application since the first was not successful.

There has been grumbling among Magu residents arguing that the area which the government has declared a game reserve is theirs hence seek change of land usage. The Magu District Council Natural Resources and Tourism Department claims that the area is reserved for game reserve and anyone who will carry agricultural activities will face the wrath of the law.

The Magu District Council Acting Forest Officer, Chami Walwa, noted that Sayaka Forest is government forest since 1996, that’s why the forestry officials destroyed crops that had been planted along Simiyu banks, and those who admitted to have intruded the game reserve paid 500,000/- fines each.