UTANGULIZI
Umoja
wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa
kutengeneza faida, wenye malengo ya jumla ya kuwaweka pamoja wananchi wote wa
Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelimisha na
Kuhamasisha wananchi kuendeleza Utamaduni na Tabia ya kufanya Kazi kwa
ushirikikiano unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha
bora kwa watu wote katika familia na jamii kwa ujumla ili kujenga Amani,Umoja,
Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi, Utawala Bora, na Mazingira Nadhifu
katika Jamii.
 |
Wanafunzi wenye uhitaji wa kusomeshwa kutoka shule ya Sekondari Itumbili. Kutoka kushoto ni Anastazia Costantine, Samuel Wanga na Emanuel Wilson Maningu walipokutana na wanakamai wa MDI |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
.JPG) |
Hapa wanakamati wetu wakiwa wamefika katoka shule ya Sekondari Itumbili na kukutana na Mwalimu Seif ambaye alikuwa anakaimu Madaraka ya Mwalimu Mkuu wa shule. Kushoto kabisa ni Dr Frank Mganga na Kulia kabisa ni King Sele |
WALENGWA
Walengwa
wakubwa wa mpango huu ni wanafunzi watatu (3) wa sekondari za kawaida (O-level)
wenye uwezo kimasomo darasani lakini wanaotoka katika familia zisizo na uwezo
(Maskini)
UTEUZI
WA WAJUMBE
Jumla
ya wajumbe wawili (2) waliteuliwa kutafuta wanafunzi watatu (3) wa sekondari za
kawaida (O-Level)wenye uhitaji wa kusomeshwa ambao wanatoka katika familia
zisizo na uwezo lakini wenye uwezo shuleni ili wasomeshwe na wajumbe wa MDI.
Wajumbe hao ni King Sele na Dr. Frank H. Mganga.
 |
Hapa ni wakati mazungumzo yakiendelea kati ya wanakati King Sele Kulia na Dr. Frank katikati na mwanafunzi Samueli Wanga |
 |
Wanakamai na mwanafunzi wakiendelea na mazungumzo zaidi |
 |
Dr Frank na King Sele wakichukua Taarifa za Mwanzafunzi Wanga |
 |
Mwanafunzi Anastazia Costantine |
 |
Mwanafunzi Emanuel Wilson Maningu |
UTEKELEZAJI
Wajumbe
walianza kazi yao kwa kuzitembelea shule za sekondari za Magu Sekondari na
Itumbili sekondari ambapo walibaini idadi ya wanafunzi sita (6) ambao
walionekana kuwa na uhitaji kwa kukizi vigezo vilivyokuwa vimewekwa na wadau wa
MDI. Kamati hii ilifika tena shule ya sekondari ya Magu tarehe 18/01/2013
nakukutana na wanafunzi hao, viongozi mbali mbali wakiwemo walimu wa shule hiyo
na mlezi wa vijana katika shule hiyo. Tarehe 18/02/2013 kamati ilifika shule ya
Sekondari Itumbili na kukutana na wanafunzi wenye uhitaji.
 |
Mwanakamati King Sele |
 |
Mwanakamati Dr Frank H Mganga |
 |
King Sele |
 |
Dr. Frank H Mganga |
 |
Mwanafunzi Samwel Wanga |
 |
Mwanafunzi Samuel Wanga |
 |
Dr Frank Mganga |
 |
Dr Frank akiwa na Kaimu Mkuu wa shule ya Sekondary Itumbili |
.JPG) |
Wanakamati waliteta jambo na Kaimu Mkuu wa Shule ya Itumbili |
HITIMISHO
Kama
ilivyooneshwa hapo juu, zoezi la upatikanaji wa wanafunzi hao linaendelea
vizuri na wanafunzi wanatarajiwaa kuwa wamepatikana mpaka mwisho wa mwezi Machi.
No comments:
Post a Comment