BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limesisitiza kuwa Juliana Shonza amevuliwa nafasi aliyokuwa akiishikilia ya umakamu mwenyekiti wa baraza hilo baada ya kukamilisha taratibu zote za kumuondoa. Kauli hiyo imekuja kufuatia Shonza kunukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema yeye bado ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa maelezo kuwa hakuwa amepewa barua yoyote ya kumsimamisha. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche alisema Shonza alitumiwa barua ya kumvua nafasi hiyo kwa njia ya posta januari 6, hata hivyo amekuwa akikataa kuipokea.
“Lakini
sio hivyo tu siku aliyokuwa anazungumza na vyombo vya habari,
tulimtumia barua akakataa kuipokea, taratibu zinatuambia kumpatia barua
lakini kama ameikataa bado haiwezi kubadili maamuzi ya chama,”alisema
Heche.
Baada ya kumtafuta Shonza ili kutoa ufafanuzi juu ya tarifa za kupokea kwa barua hiyo zilishindikana.
Siku
mbili zilizopita Shonza alikunukuliwa kwenye vyombo vya habari akisema
kikao cha kamati ya utendaji cha Bavicha kilichokutana na kupitisha
umamuzi wa kumfukuza kilikuwa sio halali huku akiwatupia lawama Heche na
Mwenyekiti wa Chama hicho Freemon Mbowe kwa madai ya kumdhalilisha.
Shonza
alisema yeye bado ni Makamu Mwenyekiti wa Bavicha na mwanachama halali
wa chama hicho. Aidha alisema anafanya mkakati wa kuwashtaki wale
anaowalalamikia kwa kumuita msaliti ndani ya chama hicho.
Shonza
alimtuhumu Heche kutengeneza mipango ya kutukuza ukanda waziwazi ndani
ya chama hicho huku akiwataka kutoa ufafanuzi wa kikatiba juu ya shutuma
zinazotolewa dhidi yake.
Habari na Kelvin Matandiko
Chanzo - Mwananchi
No comments:
Post a Comment