Wanamagu tuliopo kwenye jukwaa
hili nawasalimu katika jina la BWANA. Wale wa dini ya upande wa pili Asylam
Alykum. Tukiwa ni watu ambao tunataka maendeleo ya kweli MAGU ni lazima tuanze
kubadilika na kuwa ni watu tunaopiga hatua siku hadi siku ili mwisho wa siku
tufike ile nchi ya ahadi ya asali na maziwa. Kwa ufupi ni kuwa ili tupate
maendeleo ni lazima tuanze utaratibu ambao utawalazimisha viongozi wa serikali,
viongozi wa dini zote, viongozi wa koo (kama wapo), watu wenye ushawishi kuja
katika Jukwaa hili muhimu ili kujibu hoja zetu moja baada ya nyingine, kwani
naamini ni kwa kushirisha viongozi hawa ndipo tuweza kupenyeza michango yetu ya
maendeleo.
Nadhani sasa imefika wakati wa
kuwafahamu viongozi wetu wote wa kisiasa na wataalamu mbalimbali wanaohudumu
katika Wilaya yetu ya MAGU, tuwajue na ikiwezekana tuwajadili mmoja baada ya
mwingine MAZURI yao na MADHAIFU yao kutokana na kazi wanazofanya pale Wilayani.
Tutaje viongozi wetu kuanzia na wa juu kabisa Kiwilaya ambaye nadhani ni Mkuu wa
Wilaya mpaka wa chini kabisa ambaye nadhani ni Mwenyekiti wa Mtaa.
Baada ya hapo tutafute wakati
muafaka wa kuwaita katika Jukwaa hili wale wanaohitaji ushirikiano wetu ili
tuwaulize maswali mbalimbali na kuyajibu moja kwa moja na lengo likiwa kuwaweka
karibu na wananchi wanaowaongoza. Aina ya utaratibu huu tayari imeshaanza
kufanywa kwenye Wilaya zingine Tanzania kama vile Kilosa, Rombo, Himo na
Karagwe kwa kutaja chache, na tayari imeanza kutoa matunda.
Naamini kwa kufanya hivi ni
dhahiri tutakuwa tunalifanya kundi letu hili la UMOJA kuwa ni moja ya makundi
ambayo yapo kipekee na lenye kutimiza MALENGO yake ya MAENDELEO kwa wakati kwa
ajili ya WANAMAGU. Nianze kwa kumtaja Mkuu wetu wa Wilaya anaitwa JACQULINE
LIANA. Huyu nafikiri mnamfahamu, amerithi nafasi ya mkuu wa wilaya yetu
aliyepita aitwaye………………
TWENDE KAZI TAFADHALI. PAMOJA
TUNAWEZA
No comments:
Post a Comment