12 May 2012
Taarifa
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) , imewaacha
katika vilio na simanzi baadhi ya watumishi wa wilaya ya Magu baada ya
kuadhibiwa kwa kukatwa tozo ya asilimia 15 kama adhabu kutokana na uzembe
ulionyeshwa kwenye taarifa zao za fedha.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Cornel Ngudu-ngi, alisema kuwa
taarifa iliyotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Augustino Lyatonga Mrema Machi 29, mwaka
huu, ilibaini kuwepo kwa makosa mbalimbali ya kitabu cha mahesabu cha
halmashauri yakiwemo ya kiuchapaji, yale ya kujumlisha tarakimu na makosa
ya kujumlisha tarakimu.
Ngudu-ngi
licha ya kukanusha kuwa halmashauri yake haijahusika na ubadhirifu wa kiasi cha
Sh. bilioni 17 kama ambavyo iliripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari,
lakini alikiri kuwepo kwa mapungufu makubwa kwenye taarifa yao ya fedha hatua
iliyoifanya ofisi ya CAG kutoa adhabu ya tozo ya asilimia 15 kwa baadhi ya
watumishi wa halmashauri hiyo.
“Baada
ya kubainika kwa makosa hayo kwa mujibu wa taarifa ya CAG, tuliagizwa na LAAC
tuandae upya mchanganuo wa mahesabu yetu kwa usahihi ambapo tulifanya
hivyo na tuliwasilisha mahesabu yetu kwa CAG tangu Aprili 28, mwaka huu,
lakini mimi na wakuu wangu wa idara tuliandikiwa barua za onyo zilizoelekeza
tukatwe tozo ya asilimia 15 ya mishahara yetu ya mwezi wa nne ambayo tayari
imeishakatwa,” alikiambia kikao cha baraza la madiwani na kuongeza:
“Kitabu chetu cha mahesabu cha Magu hakikujadiliwa na kamati, hivyo siyo kweli
na siyo sahihi kusema kuwa kitabu kilionyesha upotevu wa Shilingi bilioni 17.”
Kwa mujibu wa ripoti ya LAAC iliyotolewa na Mkurugenzi wa
wilaya Ngundu-ngi, imeyataja baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na kushindwa
kuandikwa vyema kwa tarakimu za fedha Sh 81,376,625.97 ambayo iliweza kuandikwa
Sh. 81,276,626.17, ukoseaji wa majina na vyeo, likiwemo jina la Mkurugenzi
Mtendaji wa Hamashauri hiyo ambalo lilisomeka Ndugu-ngi badala ya Ngudu-ngi na
kuwepo na maelezo ya aina tofauti tofauti yaliyohusika katika kufanya manunuzi
kadhaa ya halmashauri.
No comments:
Post a Comment