Hapa mjumbe wa MDI Dr. Frank akitafakari jambo wakati wa mazungumzo na mlezi wa wanafunzi Magu Sekondari |
Mlezi wa Vijana Magu Sekondari Mwalimu Biseco |
Wajumbe wa MDI kutoka kulia, King sele na Dr. Frank H. Mganga wakimsikiliza kwa makini Mlezi wa vijana Magu Sekondari Mwalimu Biseco |
Wajumbe wa Kamati ya MDI kutoka kushoto ni Dr. Frank H. Mganga na King sele Kulia |
Mjumbe wa MDI King sele akifuatilia jambo katika document ambayo inaonesha wanafunzi mbalimbali katika shule ya Magu Sekondari |
Wajumbe wa MDI wakiwa na Mlezi wa vijana Mwalimu Biseco |
UTANGULIZI
Umoja
wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa kutengeneza
faida, wenye malengo ya jumla ya kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya
Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelemisha na Kuhamasisha wananchi
kuendeleza Utamaduni na Tabia ya kufanya Kazi kwa ushirikikiano unaojenga uwezo
wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha bora kwa watu wote katika familia
na jamii kwa ujumla ili kujenga Amani,Umoja, Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi,
Utawala Bora, na Mazingira Nadhifu katika Jamii.
WALENGWA
Walengwa
wakubwa wa mpango huu ni wanafunzi watatu (3) wa sekondari za kawaida (O-level)
wenye uwezo kimasomo darasani lakini wanaotoka katika familia zisizo na uwezo
(Maskini)
UTEUZI WA WAJUMBE
Jumla ya wajumbe
wawili (2) waliteuliwa kutafuta wanafunzi watatu (3) wa sekondari za kawaida
(O-Level)wenye uhitaji wa kusomeshwa ambao wanatoka katika familia zisizo na
uwezo lakini wenye uwezo shuleni ili wasomeshwe na wajumbe wa MDI. Wajumbe hao
ni King Sele na Dr. Frank H. Mganga ambao walipewa muda mwezi mmoja (1) wa
kutekeleza zoezi hilo.
UTEKELEZAJI
Wajumbe walianza
kazi yao kwa kuzitembelea shule za sekondari za Magu Sekondari na Itumbili
sekondari ambapo walibaini idadi ya wanafunzi sita (6) ambao walionekana kuwa
na uhitaji kwa kukizi vigezo vilivyokuwa vimewekwa na wadau wa MDI. Kamati hii
ilifika tena shule ya sekondari ya Magu tarehe 18/0/2013 nakukutana na wanafunzi
hao, viongozi mbali mbali wakiwemo walimu wa shule hiyo na mlezi wa vijana
katika shule hiyo.
HITIMISHO
Kama
ilivyooneshwa hapo juu, soezi la upatikanaji wa wanafunzi hao linaendelea
vizuri na wanafunzi wanatarajiwaa kuwa wamepatikana mpaka mwisho wa mwezi
Januari 2013.
No comments:
Post a Comment