Tuesday, March 19, 2013

Je unajua siri ya vazi la hijabu na nikabu?

KUNAMAVAZI mengi na ya kila aina yanayovaliwa na wanawake mbalimbali duniani lakini vazi la hijabu ni vazi pekee lenye sifa ya kutunza mwili wa mwanamke.
 Kumekuwa na kawaida ya watu wengi kuamini kuwa vazi la nikabu na hijabu ni kwaajili ya waislamu,leo naomba niseme kwamba siyo lazima anayevaaa nikabu na hijabu awe ni muumini wa kislamu.
Unatakiwa kuelewa kwamba kuvaa stara si kwa muislamu bali kila mwanamke anatakiwa kuvaa nguo inayofunika maungo ya mwili wake ili kuweka mwili wake katika mazingira mazuri.
Maria Sadock ni mmoja kati ya wanaweka wa Kiristo ambaye anavaa hijabu na nikabu ili kufanya ngozi yake isipigwe na jua na kuifanya kuwa nyororo. Sadock alisema kwa kipindi kirefu alikuwa akitafuta jinsi ya kufanya mwili wake kuwa na rangi moja pamoja na ngozi nyororo.
“Nilikuwa nikiangaika na mwili wangu wakati mwingine nilikuwa nikishangaa kuona rangi mbili nikadhani nina tatizo ila baadae nikagundua kuwa mwili ukiuacha wazi sana jua linaunguza ngozi,”alisema Sadock.
Katika hali ya kawaida wanawake wengi wameshindwa kutunza mili yao na kuiweka kwenye muonekano mmoja na kudhani kuwa kupaka kemikali kutaweza kufanya ngozi zao kuwa nyororo.
Mwonekano wa vazi la hijabu kwa mwanamke
Nivyema kutafuta njia zilizo salama katika kutunza miili yenu kwani kupaka vitu vyenye kemikali husababisha madhara makubwa katika ngozi na mara nyingine uleta magonjwa ya kansa na magonjwa mengine ya ngozi.
Kuhifadhi mwili kwa nguo zenye stara pia humsaidia mwanamke aonekane mwenye heshima kwani hajaacha maungo yake wazi.
Kuna njia nyingine nyingi kama kuvaa shuruali na soksi huku kwa juu ukiwa umevaa shati lenye mikono mirefu pia husaidia kuweka mwili kuwa na rangi moja kutokana na sehemu hizo kutokuwa wazi.

No comments:

Post a Comment