MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Wilfred Lwakatale amenyima dhama katika kesi yake ya Ugaidi
ilisomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Katika kesi hiyo Lwakatale na mwenzake Ludovick Rwezahura Joseph
wamefikishwa katika Mahakama wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la
kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhulu
Dennis Msacky.
Akisoma hati ya mashtaka leo mbele
ya Hakimu Mkazi, Emillius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Puldens
Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda
makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
![]() |
Mshtakiwa wa pili katika kesi ya Lwakatale Ludovick Rwezahura Joseph aliyenyoosha vidole viwili |
Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28, mwaka jana katika eneo la
King’ong’o Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama
kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhulu Dennis Msacky kinyume na kifungu cha
227 cha sheria ya kanuni ya adhabu. Wakili
huyo wa serikali katika shtaka la pili alidai kuwa washtakiwa hao kwa
pamoja walikula njama ya kufanya kosa la jinai kinyume na kifungu cha
sheria cha 24 (2) cha sheria dhidi ya ugaidi sura ya 21 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment