MSAFARA wa Rais Jakaya Kikwete ambaye yupo katika ziara yake ya
kikazi jijini Dar es Salaam umedaiwa kusababisha kifo cha askari wa
usalama barabarani Kopro Elikiza Nko aliyekuwa akiongoza magari eneo la
barabara ya new Bagamoyo mkabala na ofisi za TBC na Barabara ya
Shekilango.
Habari
zimeeleza kuwa msafara huo ulikuwa na magari yasiypungua 40 ikiwa katika
mwendo kasi jambo ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa
ajali hiyo.
Shuhuda mmoja aliyetupasha habari amesema askari huyo kabla ya
msafara kuanza kupita alisimamisha magari yaliyokuwa upande mwingine na
baada ya magari hayo kusimama naye aliondoka eneo la barabara na
kupisha msafara huo.
"Trafic huyo baada ya kuona muda unazidi kwenda na magari yanazidi
kuongezeka alihisi labda msafara wa Rais umeshamalizika ila magari
yanayoendelea kwenda ni yaliyounga kwenye msafara huo jambo ambalo ni
kinyume na sheria"alisema shuhuda wa ajali hiyo"nakuongeza:
"Baada ya kuingilia kati na kuanza kuruhusu gari za upande mwingine
ndipo ilipotokea gari ambayo ilikuwa kwa kasi sana na kusababisha ajali
hiyo ambapo marehemu aliweza kufariki palepale.
Shuhuda huyo amesema kilichowashangaza wengi ni kuona kuwa gari za
msafara wa rais zimesababisha kifo lakini hazikusimama ili kutoa msaada
kwa askari huyo badala yake ziliendelea na ziara hiyo".
![]() |
Wasamaria wema wakiufunika mwili wa askari aliyegongwa na gari kwenye msafara wa rais na kufariki hapohapo |
Akizungumza na waandshi wa habari Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kinondoni,Charles Kenyela alikiri kuwepo kwa taarifa hizo na
kusema kwamba askari huyo aligongwa na gari ambalo haikuwa kwenye
msafara huo. "Nikweli askari huyo
amefariki katika ajali hiyo, lakini hakugongwa na gari iliyokuwa kwenye
msafara bali ajali hiyo imesababishwa na gari aina Land Rova
inayomilikiwa na Kanisa la Assemblies Of God (TAG) na tayari jeshi la
polisi limeanza kumtafuta dereva wa gari hilo"alisema Kenyela.
No comments:
Post a Comment