Tuesday, March 19, 2013

Mbowe: Chadema hatuhusiki utekaji wa mwandishi Kibanda

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara hivi karibuni


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amekanusha vikali kwamba tukio lililomkuta Mwandishi wa habari Absalom  Kibanda halikufanywa na chama chake bali watu wasio na mapenzi mema na chama hicho wamelenga kukipaka matope.
Akizungumza wakati akiwahutubia mamia ya watu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom mkoani Shinyanga Mbowe amesema mpango wa uchochezi na utekaji aliofanyiwa Kibanda usihusishwe na suala la mwanachama wake Alfred Lwakatare.
"Sisi hatunamuda wa kumteka mtu, watu wanadai kuwa tumemteka Kibanda, ili iweje sasa, hatuna kikosi chochote cha silaha, hawa ni baadhi ya watu wanaotaka kukipaka matope chama,"alisema Mbowe.
Aidha Mbowe alierndelea kutoa hisia zake kuwa hoja yao ya kutaka kufanya maandamano nchini nzima ili waziri wa Elimu  ajiuzulu ipo palepale na kwamba kwa sasa wapo katika maandalizi.

No comments:

Post a Comment