![]() |
Lema akiwa na sidi yenye waraka wa Rais Kikwete |
WAKATI mwingine unapaswa kupewa pole na kuombewa na kufanyiwa dua
kwani wewe ndie unatumikia ofisi kubwa kuliko zote Nchini na wakati huo huo
unapaswa kupewa hongera kufikia malengo yako hayo ya kutumikia ofisi kubwa na
ya Heshima kuliko zote Nchini.
Nimekuwa nikitafakari sana suala la Udini katika Taifa letu na huko nyuma
mwaka jana nilikuandikia pia waraka kuonya na kukumbusha hatua mathubuti kabla
mambo hayajaharibika sijui kama ulisoma lakini naamini Usalama wa Taifa ambao
siku hizi wanatumikia CCM watakuwa walisoma.
Nape na wenzake pia walipata fursa ya kuusoma,Mh Rais katika waraka hule
nilisema hivi “ Mh Rais Taifa linahitaji Tiba “ siwezi leo kuandika kile
nilichosema katika waraka ule ila niliweza kubashiri sumu ya udini inayoendelea
katika Taifa lako na langu, Mh Rais , ukweli nakwambia ukifanya mchezo kidogo
sana Taifa hili linapotea likiwa mikononi mwako kwani hali ya nchi sio nzuri
hata kidogo na watu waliokuwa wanaishi kwa umoja na upendo sasa wanaanza
kutafuta mbinu za kugombana na kuuwana.
Mh Rais, Siasa ya Udini na Ukanda makusudi yake yalikuwa kudhoofisha vyama
vya upinzani na yalifanikiwa kwa baadhi ya vyama kudhoofishwa sana na mkakati
huo unaendelea dhidi ya Chadema lakini kinachosikitisha ni kuwa wale waliobuni
mkakati huo walishindwa kutafakari au kuona madhara yake mbele .
Mh Rais, mkakati wa kudhoofisha Chama cha Siasa kwa Udini na Ukanda hauishi
tu kuangamiza hicho Chama bali kuwagawa Watu na Taifa kwa Ujumla , Mtu
anapojaribu kusema Chadema ni Chama cha Wakristo kimsingi matamshi hayo
hayaangamizi Chadema tu bali yanagawa Watu kwa matabaka ya Udini wao na kufanya
Dini moja iamini kuwa Dini nyingine ni mbaya na hivyo mpango huo unafanya Watu
waanze kutazamana kwa Udini na Ukabila na matokeo yake ndiyo haya tunaanza
kuyaona leo .
Mh Rais, Taifa linahitaji tiba , Hivi karibuni Waziri Mkuu alienda Geita
kwenye mgogoro wa Waisilamu na Wakristo na niliona mawazo ya Waziri Mkuu kwenye
vyombo vya habari na kwa kweli nilisikitika kwa busara zile zilizokuwa zimejaa
hofu kubwa . Tatizo lile lilianza na nani kati ya Mkristo na Muislamu
anayepaswa
Mh Rais , Nilipoona jambo hili nilianza kujiuliza maswali mengi sana, kwanza
, umakini huu kwa pande zote mbili juu ya jambo hili umeletwa na nini na nani?
Kwani yako mambo mengi yaliyokatazwa na Biblia na Msaafu ambayo watu wote wa
dini hizi mbili wamekataa kuyatii au kuyafuata , kwa mfano waislamu na wakristo
vijana kwa wazee wanakunywa pombe pamoja baadhi yao kujenga mahusiano hata ya
kimapenzi yasiyo rasmi bila hata kufuata utaratibu wa Msaafu wala Biblia lakini
hapa hutaona ugomvi mkubwa sana japokuwa ni masuala yanayo mkera na kumuudhi
mwenyezi Mungu sana.
Mh Rais , ndio maana katika suala hili la nani achinje kati ya Muislamu na
Mkristo niliposikia maafa yake nikakumbuka waraka niliokuandikia mwaka jana
kuhusu choko choko za Udini ambazo zimeanza kuleta maafa ambazo Mwanzilishi
wake ni CCM .
Mh Rais Chama chako unachokiongoza , Team yako imekuwa ikifanya sana
propaganda hizi za, Udini , Ukabila , na Ukanda usiku na mchana , lakini
nimekuwa nikikerwa sana na Jinsi kabila la Wachaga linavyochukuliwa katika
propaganda hizi na wanaofanya hivyo asilimia kubwa ni mashemeji wa Wachaga na
mimi najiuliza wanaweza vipi kufanya Siasa za Ukanda na Ukabila wakati wao
wenyewe ni familia moja ?.
No comments:
Post a Comment