MKE wa rais Mama Salima Kikwete amewataka wanawake wajasiria
mali nchini kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo yao wenyewe pamoja
na kuhakikisha kuwa watoto wa kike wanapelekwa shule kwa ajili ya kupata elimu.
Ametoa mwito huo Wilayani Magu Mkoani Mwanza wakati
anazungumza na wanawake wajasiria mali katika Kijiji cha Kisesa pamoja na kuweka
jiwe la msingi katika Chuo cha Sanaa na Ufundi cha Bujora Wilayani Magu.
Mama Kikwete alikuwa wilayani hapa mara baada ya maadhimisho
ya siku ya wanawake duniani ambayo ilimwezesha kujionea shughuli mbalimbali za
ujasilia mali zinazofanywa na wanawake katika kijiji cha Kisesa.
Aliwataka wanawake kuongeza juhudi na kufanya kazi katika
vikundi ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa zinazokidhi viwango vya Kitaifa na
Kimataifa na hatimaye kupata soko la bidhaa zao.
Akiweka jiwe la msingi katika hosteli hizo alisema kuwa
hosteli hizo zitawasaidia watoto wa kike kuendelea na masomo katika chuo hicho
na shughuli mbalimbali za maendeleo.
Akiwa katika chuo cha Bujora, Mama Kikwete alihimiza jamii
kutunza tamaduni zao kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Watoto ni lazima wajue kuwa utamaduni wetu ni upi na nini,
tusipohifadhi hivi na hawa wazee wakiondoka, watoto watakosa historia, alisema
mama Kikwete.
Katika ziara hiyo mama Kikwete kama Mwenyekiti wa Taasisi ya
Maendeleo ya Wanawake (WAMA), ailahidi kuwapatia wanawake wajasiria mali kiasi
cha shilingi million tano, pamoja na Chuo cha Sanaa na Ufundi shilingi million tano.
Akiwa katika Kijiji cha Bujora Wilayani Magu, Mama Kikwete
alitembelea kijiji cha Makumbusho cha Bujora, ambapo alisimikwa kuwa mke wa
mtemi na kupewa jina la Ebula.
Awali wajasiria mali waliomba kujengewa uwezo wa elimu ya
ujasilia mali na pia kuwezeshwa kwa kupatiwa mitaji ili waweze kukabiliana na
changamoto mbalimbali zinazowakabili.
No comments:
Post a Comment