HATIMAYE Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema,) Wilfred Lwakatale amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka manne.
Kada huyo wa Chadema anashitakiwa kwa kosa la ya kula njama ya kumteka na kumdhuru Denis Msacky na amenyimwa dhama katika kesi yake ya Ugaidi ilisomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Katika kesi hiyo Lwakatale na
mwenzake Ludovick Rwezahura Joseph wamefikishwa katika Mahakama
wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kula njama ya kutenda kosa la
jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhulu Dennis Msacky.
Akisoma hati ya mashtaka leo mbele
ya Hakimu Mkazi, Emillius Mchauru, Wakili wa Serikali Mkuu, Puldens
Rweyongeza kuwa washtakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda
makosa ya jinai kinyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya
adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Rweyongeza alidai kuwa Desemba 28,
mwaka jana katika eneo la King’ong’o Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa hao
kwa pamoja walikula njama kwa kutoa sumu kwa nia ya kumdhulu Dennis
Msacky kinyume na kifungu cha 227 cha sheria ya kanuni ya adhabu.
Wakili huyo wa serikali katika
shtaka la pili alidai kuwa washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya
kufanya kosa la jinai kinyume na kifungu cha sheria cha 24 (2) cha
sheria dhidi ya ugaidi sura ya 21 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alidai kuwa washtakiwa hao, Desemba
28,2012 walishirikiana kupanga njama za utekaji nyara dhidi ya Msacky
kinyume na kifungu cha 21 cha sheria inayopinga ugaidi.
![]() |
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema Wilfred Lwakatale akiwasalimia wafuasi wa chama hicho kwa ishara ya vidole viwili baada ya kuwasili katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. |
Katika shtaka la tatu, washtakiwa hao wanadaiwa kufanya mkutano wa
vitendo vya kigaidi kinyume na kifungu cha 5 (a) cha sheria namba 21
inayopinga ugaidi iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aliendelea kudai kuwa siku hiyo ya
tukio, washtakiwa hao walipanga na kushiriki katika mkutano wa kupanga
kitendo cha ugaidi cha utekaji nyara dhidi ya Msacky. Kwa mujibu wa shtaka la nne, Lwakatale anadaiwa kuhamasisha vitendo vya ugaidi.
No comments:
Post a Comment