Thursday, January 24, 2013

Hali ya Manumba bado tete! Sasa akimbizwa Afrika Kusini…

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai, DCI, Robert Manumba, ameondoka jana tarehe 24/01/2013 kuelekea Afrika Kusini, kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo.

Habari za uhakika zilizoifikia Magu Development zimeeleza kwamba Manumba ameondoka kwa ndege maalum ya kampuni ya AAR kwenda Afrika Kusini akitokea hospitali ya Agakhan ya jijini Dar alikokuwa amelazwa baada ya kupelekwa Uwanja wa Ndege kwa gari la kubebea wagonjwa (ambulance) maalumu.
"Hali yake imetia matumaini sasa japo bado hajitambui, na Mungu akimsaidia kufika salama, tutakuwa tumeokoa maisha yake," anasema mtoa habari wetu.
DCI Manumba alilazwa katika Hospitali ya Agakhan ya jijini Dar es Salaam kwa ambapo hali yake imekua ikiriporiwa kuwa mbaya.
Taarifa iliyothibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema kuwa Manumba alilazwa hospitalini hapo baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilisema pamoja na matatizo mengine aliyonayo, amekuwa akisumbuliwa na malaria.

No comments:

Post a Comment