Monday, February 11, 2013

HOTUBA YA PAPA BENEDICT XVI ALIYOITOA MUDA SIO MREFU KUHUSU KUSUDIO LAKE LA KUJIUZULU HIVI KARIBUNI:


"Dear Brothers,
I have convoked you to this Consistory, not only for the three canonizations, but also to communicate to you a decision of great importance for the life of the Church.

After having repeatedly examined my conscience before God, I have come to the certainty that my strengths, due to an advanced age, are no longer suited to an adequate exercise of the Petrine ministry.

I am well aware that this ministry, due to its essential spiritual nature, must be carried out not only with words and deeds, but no less with prayer and suffering.

However, in today's world, subject to so many rapid changes and shaken by questions of deep relevance for the life of faith, in order to govern the bark of Saint Peter and proclaim the Gospel, both strength of mind and body are necessary, strength which in the last few months, has deteriorated in me to the extent that I have had to recognize my incapacity to adequately fulfill the ministry entrusted to me.

For this reason, and well aware of the seriousness of this act, with full freedom I declare that I renounce the ministry of Bishop of Rome, Successor of Saint Peter, entrusted to me by the Cardinals on 19 April 2005, in such a way, that as from 28 February 2013, at 20:00 hours, the See of Rome, the See of Saint Peter, will be vacant and a Conclave to elect the new Supreme Pontiff will have to be convoked by those whose competence it is.

"Dear Brothers, I thank you most sincerely for all the love and work with which you have supported me in my ministry and I ask pardon for all my defects.

And now, let us entrust the Holy Church to the care of Our Supreme Pastor, Our Lord Jesus Christ, and implore his holy Mother Mary, so that she may assist the Cardinal Fathers with her maternal solicitude, in electing a new Supreme Pontiff. With regard to myself, I wish to also devotedly serve the Holy Church of God in the future through a life dedicated to prayer."

-BBC and Reuters

Taarifa ya Helen Kijo-Bisimba- Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Kuhusu Vurugu za Waislam na Wakristu Mkoani Geita

Tumepokea taarifa za masikitiko kuhusu vurugu zilizotokea huko Buselele Chato kuhusu uchinjaji wa nyama unaobishaniwa na Waislam na Wakristo.
Chanzo cha Habari hizi kimetueleza kuwa baada ya mivutano kuhusu uchinjaji wa nyama .Baaadhi ya Wakristo waliamua kuanzisha bucha zao ili wachinje na kununua hapo ili wasishiriki kula nyama zilizochinjwa kama sehemu ya ibada ya Kiislamu kwa vile uchinjaji kwa Waislam ni ibada. 
Baada ya kufungua Bucha hiyo leo asubuhi taarifa inasema watu wanaosadikiwa kuwa waislam walifika kutaka kuifunga hiyo Bucha na baadaye Polisi nao walifika na walitaka wamchukue mwenye bucha.
Suala hili likazua tafrani na pakatokea mapigano kati ya pande mbili yaani waislam na wakristo na kuna watu wameumizwa.Taarifa imezidi kueleza kuwa pia mali za aliyehamasisha ufungwaji wa bucha nazo zimeharibiwa. 
Baada ya kupokea taarifa hii tumewatuma waangalizi wetu wa haki za binadamu kwenda kutuletea kwa kina hali halisi kama watakavyoweza.Tunahabari kuwa kikosi cha kuzuia fujo kilifika na kutuliza hizo vurugu.Jambo tunaloliona kwa haraka ni kuwa kunaelekea kukosekana kwa uongozi wa kuyatazama masuala kama haya na kuyawekea msimamo na maelekezo kabla vurugu kama hizi kutokea. 
Pili tunaona kuwa hali ya kukosa stahamala za kidini inajengeka nchini jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama na amani hapa nchini.
Wakati tunasubiri taarifa zaidi tunapenda kutoa angalizo kwa viongozi wetu maana tumesikia mkuu wa wilaya tayari ameshafika katika eneo la tukio,Masuala kama haya yatazamwe kwa mujibu wa sheria na sheria zifuatwe lakini pia kwa kuzingatia haki za binadamu na hususani haki za kiraia na kiutamaduni ambazo zinatoa uhuru wa ibada na kila mtu asiingiliwe katika haki hizi.Lakini pia njia za utatuzi wa migogoro ya aina hii isifanywe kijuujuuu bali pawe na nafasi yamaongezi ya kina ya uchambuzi wa kiini cha mgogoro.
 Tutaweza kutoa taarifa zaidi tutakapopokea taarifa kutoka kwa waangalizi wetu wa kiini na matokeo ya mgogoro au vurugu hizi