Friday, January 18, 2013

WAKUU WA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MAGU ZILIOVURUNDA KUKIONA

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu, Bi Naomi Nnko akifafanua jambo wakati wa kikao cha kazi cha viongozi wa shule za msingi Wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Magu, Jacquiline Liana




Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Magu Naomi Nnko, amemwagiza Ofisa Elimu wa shule za msingi Yesse Kanyuma kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wa shule kumi ambazo zilifanya vibaya katika mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2012.

Nnko ambaye ni mwalimu kitaaluma alitoa agizo hilo wakati akifunguakikao cha utekelezaji wa kazi kwa walimu wakuu, walimu wakuu wasaidizi, waratibu wa elimu kata na viongozi wa elimu wilayakatika ukumbi wa CCM wilayani Magu.

“Nakuagiza Ofisa Elimu, kuwachukulia hatua walimu wakuu ambao shule zao zilifanya vibaya katika matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi na kunipa hatua uliyochukua” alisisitiza.

Aidha Mkurugenzi huyo alimwagiza ofisa Elimu huyo kuwaandikia barua za pongezi walimu wa shule za msingi 12 ambao shule zao zimefanya vizuri katika matokeo hayo ya kuhitimu elimu ya msingi.

Nnko alizitaja shule ambazo zilifanya vibaya kuwa ni pamoja na Mizwale, Malangala, Chabula, mwamachibya, Bunyanyembe, Milambi, Bugando, Misungwi, ijinga na Ng’haya.

Aidha aliwapongeza walimu wa shule 12 ambazo zilifanya vizuri ambapo alizitaja kuwa ni Isandula, Mahaha, itongo, Magu, Mwalinha, Ng’watelesha, Sesele, Ilungu, igombe, Busami, Makamba na Masangani.

Kuhusu shule ambazo hazikufanya vizuri, Mkurugenzi huyo ameagiza idara ya elimu wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina juu ya shule hizo, ambapo pia amempa Ofisa Elimu wa shule za msingi muda wa wiki mbili awe amewachukulia hatua wakuu wa shule hizo.

Hatua mojwapo aliyopendekeza kuwachukulia walimu wakuu wa shule hizo ni pamoja na kuwavua madaraka ya ualimu ukuu, na nafasi zao kuchukuliwa na walimu wengine wenye sifa nzuri kiutendaji kazi.

Wakati huohuo Mkurugenzi huyo ambaye ni mwalimu kitaaluma, alikemea

No comments:

Post a Comment