Wednesday, January 30, 2013

Migiro Mkuu wa Chuo OUT

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.
Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013

TAARIFA YA MKUTANO WA M.D.I DAR ES SALAAM ULIOFANYIKA TAREHE 27/01/2013 MARYLAND PUB, MWENGE DSM

AGENDA

1.      UTANGULIZI
2.      KUFUNGUA KIKAO
3.      KUKAMILISHA USAJILI WA UMOJA
4.      MAJUKUMU YA UMOJA KWASASA
5.      KUHAMASISHA MAWASILIANO BAINA YA WAJUMBE
6.      KUHIMIZA UTOAJI WA MICHANGO YA MWISHO WA MWEZI
7.      MENGINEYO
8.      HITIMISHO

1.      UTANGULIZI
Umoja wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa kutengeza faida, wenye malengo ya jumla ya kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelemisha na Kuhamasisha wananchi kuendeleza Utamaduni na Tabia ya kufanya Kazi kwa ushirikikiano unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha bora kwa watu wote katika familia na jamii kwa ujumla ili kujenga Amani,Umoja, Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi, Utawala Bora, na Mazingira Nadhifu katika Jamii.

2.      KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa MDI kuanzia saa Kumi na Nusu jioni, Maryland Pub, Mwenge Dar es salaam.

3.      KUKAMILISHA USAJILI WA UMOJA

Ili M.D.I iweze kujiendesha kikamilifu na kwa ufanisi ilihitajika kusajili umoja haraka iwezekanavyo ili kupata baraka zote kutoka kwenye mamlaka husika ya nchi yetu ya Tanzania. Kwa hivyo kikao kiliwateua wanachama watatu (3) wafuatao kushughulikia na kufuatilia usajili wa MDI.

  1. Juma William Yabeja
  2. Samuel Magoiga
  3. Wilbert Maige

Wanachama hawa walipewa muda wa wiki mbili  (2) kuwasilisha taarifa ya usajili huo.

Kuwa na umoja uliosajiliwa ni vizuri kwa sababu zifuatazo;

KWANZA,umoja utakuwa na nguvu kisheria ya kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo kama tulivyojipangia kama Magu Development Initiative (MDI).

PILI, itatuwezesha kutekeleza majukumu ya umoja ikiwa ni pamoja na kuweza kupata misaada ya wafadhili wa maendeleo ili kusaidia katika kuteleza malengo ya umoja.

TATU, itatuwezesha kutimiza mahitaji ya kikatiba kama yalivyoainishwa kwenye kaatiba ya MDI Ibara ya 9(10.2) inayoelekeza jinsi ya kuwa na vyanzo mbadala vya mapato ya umoja.

NNE, kama jumuiya, tunatarajia kuwa na mipango mikakati ya kukemea kwa nguvu zote dhana ya UCHAWI, Mauaji ya ALBINO, Mauaji ya VIKONGWE, na mengineyo ambayo kwa muda mrefu yamechangia kudumaza maendeleo ya wanaMagu na Magu kwa ujumla.

4.      MAJUKUMU YA UMOJA KWASASA
Kama isemavyo elimu ndio ufunguo wa maisha na wengi wetu ni mashaidi katika hili, kikao kilionelea kuwepo na mkakati maalumu na endelevu kwa ajili ya kusomesha wanaMagu walio na mahitaji (wanaotoka katika familia masikini). Kwa hiyo kutakuwa kunafanyika FUND RAISING kila mwaka kwa ajiri ya kusomesha wanafunzi hao.

Zaidi tulishukuru Mwana Magu mmoja aitwaye WILBERT MAIGE katika kikao hicho kwa kujitolea kusomesha mwanafunzi mmoja mwaka huu (2013) kutoka shule ya sekondari ya kata ya SUKUMA. Kwa hili bado mlango upo wazi kwa ajili ya mdau yeyote atakayeguswa kujitokeza kwa ajili ya kusaidia wadogo zetu wapate elimu dunia.

5.      KUHAMASISHA MAWASILIANO BAINA YA WAJUMBE WA MDI
Pamoja na wajumbe wengi kujuana kupitia facebook tu tulionelea kwamba umefika wakati mwafaka wa wanaM.D.I kuwa tunakutana ktk vikao sehemu mbalimbali tulipo ili tuzidi kufahamiana zaidi kama wanafamilia moja iitwayo (WANAMAGU). Tunaangalia uwezekano wa kupata kiongozi kila Mkoa na Wilaya zetu kwa ajili ya kufanikisha jambo hili.

6.      KUHIMIZA UTOAJI WA MICHANGO YA MWISHO WA MWEZI
Kikao kilionelea kuendelea kuwaomba wajumbe kujitokeza zaidi kwa ajili ya kutoa ada hii ambayo itatumika kujenga M.D.I na sisi pia. Matumizi yake yatolewa kila hela itakapotumika kwa ajili ya shughuri za M.D.I. Kiasi kilichobaki kitawekwa kwenye akaunti yetu No. 01J209830000 CRDB BANK.

7.      MENGINEYO

KWANZA, Kuweka ajira zote zinazotolewa katika vyombo vya habari ndani ya M.D.I ili wadau wapate kuziona na kuomba kazi hizo.
PILI, Kuwa na ofisi kuu Dar Es salaam kama ilivyoainishwa kwenye Katiba.

8.      HITIMISHO
Kama wanamagu na wanachama wa umoja huu wa MDI, tuna jukumu la msingi la kushiriki katika shughuli za kukuza umoja wetu na pia katika shughuli zake kwa kujitoa kwa dhati kimaarifa, muda, kirasilimali na juhudi.

Nawatakia kushiriki kwema kuijenga Magu Mpya.

MAENDELEO YA MAGU…PAMOJA TUNAWEZA

Sunday, January 27, 2013

TAARIFA YA MAENDELEO YA UTOAJI WA MCHANGO WA MWISHO WA MWEZI KWA MWEZI JANUARI MPAKA TEREHE 28/01/ 2013

UTANGULIZI

Umoja wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa kutengeza faida, wenye malengo ya jumla ya kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania kwa dhumuni la Kuelemisha na Kuhamasisha wananchi kuendeleza Utamaduni na Tabia ya kufanya Kazi kwa ushirikikiano unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta mabadiliko ya maisha bora kwa watu wote katika familia na jamii kwa ujumla ili kujenga Amani,Umoja, Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi, Utawala Bora, na Mazingira Nadhifu katika Jamii.

Suala la michango ya kila mwisho wa mwezi linatokana makubaliano katika jukwaa hili kuwa michango hii itakuwa inarudi kwa wanachama kwa njia nyingine na kiasi kilichobaki kinatunzwa katika akauunti ya umoja kwa ajili ya matumizi mengine kadiri itakavyoonekana sawa kwa mujibu wa Katiba yetu ya MDI ya mwaka 2009.

Nitumie nafasi hii pia kuwakumbusha kuendelea kushiriki katika mijadala ya uchangiaji wa mawazo  katika jukwaa hili kwa kuwa mpaka sasa zawadi ya mwisho wa mwezi ipo tayari na inasubiri mshindi tu.

WALIOLIPA MICHANGO YAO MAPAKA SASA

Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hili Bw. Juma William naomba kutoa taarifa kuwa, mpaka sasa tumefanikiwa kukusanya michango ya mwisho wa mwezi katika wiki ya Nne ya mwezi Januari 2013 kutoka kwa wajumbe wafuatao;

1.       Mussa Budodi-------------------> Tshs. 2,000/=
2.      Frank H Mganga---------------->Tshs. 2,000/=
3.       Abel Daud Nitwa---------------->Tshs. 2,000/=
4.       Machibya Anthony Matulanya------->5,000/=
5.      Martin Mambosasa---------------------->2,000/=
6.       Juma William Yabeja------------------>2,000=
7.      Simon Kahindi--------------------------->2,000/=
8.      Obeid Mashauri------------------------->>2,000/=
9.      King Sele---------------------------------->2,000/=
10.  Wilbert Maige--------------------------->5,000/=
11.  Lucas Katemi Matulanya--------------->2,000/=
12.  Simon Makungu------------------------->2,000/=
13.  Samuel Magoiga------------------------>2,000/=
14.  Felician Kanani--------------------------->2,000/=

Na wengine bado wapo katika hatua za ahadi kutekeleza hilo. namba yetu ya M-PESA ni 0753544084 ambayo imesajiliwa kwa jina la Mwenyekiti JUMA YABEJA. Kumbuka tumebakiwa na siku mbili (2) tu kabla ya kuanza mwezi mpya.

Nawasilisha.

HITIMISHO

Taarifa hii pia inapatikana kwenye Facebook Group yetu http://www.facebook.com/groups/mdi2009/.

Nawatakia Utekelezaji Mwema.

Maendeleo ya Magu..............................Pamoja Tunaweza

Thursday, January 24, 2013

Wanafunzi, walimu kujisadia vichakani ni aibu ya taifa

 CHANZO NIPASHE
Katika toleo la jana 24/01/2013 la gazeti hili ukurasa wa 16 kulikuwa na habari ya kuchefua, kukasirisha na kukatisha tamaa, kwamba wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Nampemba iliyopo Kata ya Nambambo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na kujisaidia vichakani kwa kukosa vyoo.

Habari hiyo ilisema kuwa shule hiyo ya kijiji cha Nampemba iliyojengwa kwa msaada wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) haina vyoo kwa kipindi cha miaka saba, hali hiyo inawaacha wanafunzi na walimu wao kujisitiri vichakani. Yaani ndani ya miaka 51 ya Uhuru bado hatuwezi kujenga choo!

Hakuna binadamu yeyote mstaarabu ambaye hajui maana ya kuwa na choo na kukitumia. Hakuna. Hali inakuwa ni ya kushangaza na kuchefua zaidi kundi linalokuwa halina choo kuwa ni la wanafunzi na walimu, yaani shule ambayo inapaswa kuwa kitovu cha ustaarabu na kuelemisha jamii juu ya madhara ya kutokuwa na choo, ndiyo inakosa huduma hiyo muhimu kwa afya ya binadamu.

Ni hakika kama walimu na wanafunzi hawa hawajaanza kuugua magonjwa ya milipuko kama kuhara, kipindupindu na mengine ya tumbo, basi wana bahati ya mtende kwa kuwa kujisaidia ovyo vichakani ni sawa kabisa na kuendelea kuukaribisha uchafu huo kwenye vyakula na maji wanayotumia.

Katika eneo lote la nchi hii hakuna hata kipande cha sentimeta moja ambacho hakina kiongozi.

Kila ukikaribia wakati wa uchaguzi watu wanapigana vikumbo kusaka uongozi wa kuchaguliwa, hawa ni kuanzia wajumbe wa kamati za utawala ngazi ya vijiji na mitaa, wenyeviti wao na kuna watendaji wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi. Hawa ni watendaji wa vijiji, mitaa na kata. Hawa ndiwo wasimamizi wakuu wa shughuli za maendeleo katika maeneo yao. Wapo wamejaa lakini hawafanyi lolote!

Mbali na viongozi hao, shule hii ina walimu, yupo mwalimu mkuu, wapo wanafunzi ambao wana wazazi. Wote hawa kwa ujumla wao kwa miaka saba wameshindwa kujenga choo cha shimo katika shule hii ili wanaotoa huduma na kuhudumiwa na shule hii waishi maisha ya staha kwa kuwa na mahali pa kujisitiri.

Mara nyingi tumejiuliza maswali ambayo majibu yake hayapatikani kwamba hivi hawa wanaokimbilia kusaka madaraka ya uongozi katika nchi hii kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi juu baadhi yao wanakuwa wanawaza nini? Ni kutumika au kutumikiwa?

Inashangaza kuona kwamba eti
mwenyekiti wa kijiji hicho bila aibu anakwepa wajibu wa kazi hii kwa kuitupia lawama Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa madai kuwa ndiyo chanzo cha ukosefu wa choo katika shule hiyo.

Kwamba kijiji kizima kwa miaka saba kimeshindwa kujenga choo cha shule, ni utetezi unaoacha maswali magumu ya uwajibikaji kwa watu wanaosaka madaraka ya umma, lakini wakishakalia viti hivyo hawana wanalofanya mbali ya kuendekeza ubinafsi.

Kadhalika, kama kijiji kinaweza kuruhusu shule iendeshwe bila choo, inatupa hofu kwamba hata wanavijiji kwa ujumla wao suala la vyoo siyo la kipaumbele katika maisha yao; tunajiuliza kama makazi yao yana vyoo vya kueleweka. Hofu hii inapata mashiko kwa sababu kama wangelikuwa wanajua umuhimu wa vyoo kiasi hicho, basi wasingelikubali kuona shule wanayosama watoto wao ikiachwa katika ukiwa kama huo.

Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea hakina tunakosa maneno ya kusema, kwamba miaka saba imeshindwa kuisaidia shule ya msingi kuwa na choo? Katika nchi zinazojali uwajibikaji baraza zima la madiwani na mkurugenzi wa halmashauri walipaswa kuachia hazi kwa uzembe huu ambao unakera na kutia kichefuchefu.

Tunajiuliza maswali mengi kama kweli hatuwezi kujenga choo na kukitumia kwenye shule zetu, hivi tunaweza kutoa elimu ya namna gani basi? Tunakua na ujasiri gani wa kuamini kwamba tunaweza kushindana katika dunia hii inayosukwasukwa na changamoto za utandawazi na maendeleo ya teknolojia ya kompyuta?

Itoshe tu kusema kuwa Halmashauri ya Nachingwea, wanakijiji na uongozi mzima cha Nampemba na uongozi shule ya msingi hiyo hakika wanaidhalilisha Tanzania kwa kuishi bila choo. Hali hii kwa ukweli haikubaliki na ni moja ya kipimo cha chini kabisa wote wanaojiita viongozi kwenye mnyororo wa madaraka kuanzia halmashauri, kijijini na shuleni kuwa wameshindwa kazi.

Kama kiongozi hawezi kusimamia ujenzi na matumizi ya choo kwenye eneo lake la utawala hivi anaweza kufanya nini basi kama kiongozi?

CHANZO NIPASHE.

Tas Mwanza yalaani albino kuzikwa ndani ya duka

Chama  cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi (Tas) mkoani Mwanza, kimelaani vikali kitendo cha familia moja wilayani Magu kumzika ndani ya chumba cha biashara mtoto wao mwenye ulemavu wa ngozi (albino).

Mtoto huyo aliaga dunia Desemba 15, mwaka jana nyumbani kwao mjini Magu.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mwenyekiti wa Tas Mkoa wa Mwanza, Alfred Kapole, alisema kimsingi chama chake hakikubaliani na kitendo hicho ambacho kilifanyika usiku wa manane bila kuishirikisha jamii ya eneo husika.

Kapole, ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wenzake wa chama hicho mkoani Mwanza na taifa, alisema hatua yao ya kulaani kitendo hicho inatokana na ukweli kuwa inaweza kuchochea mauaji dhidi ya albino.

Alifafanua kuwa wiki iliyopita, alipokea taarifa kutoka wilayani Magu kuwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Witness Edward Omari, mwenye umri wa miaka miwili na miezi saba, mkazi wa mtaa wa Isandula mjini Magu, amefariki dunia na mwili wake kuzikwa ndani ya chumba cha biashara kinachomilikiwa na baba yake.

Aidha, alisema taarifa hizo zilieleza kuwa siyo tu kwamba mtoto huyo alizikwa ndani ya chumba cha duka, bali pia kitendo hicho kilifanywa usiku wa manane bila jamii ya eneo husika kushirikishwa.

“Nilipigiwa simu na mwenzetu mmoja kutoka Magu akaniambia kwamba baada ya Witness kufariki dunia, alizikwa ndani ya chumba cha duka, na kweli tulipokwenda kuitembelea familia yake, tuliingizwa ndani ya chumba hicho kuonyeshwa kaburi lake,”alisema Kapole.

Aliongeza kwamba taarifa zaidi walizozipata zinasema kuwa mwili wa mtoto huyo ulichukuliwa na wazazi wake kutoka chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Wilaya ya Magu Desemba 16, mwaka jana  majira ya usiku kwa ajili ya kwenda kuuzika.

Ofisa Uhusiano wa Tas taifa, Josephat Toner, alisema wao kama jamii ya albino, hawakubaliani na kitendo hicho kwa sababu kinakiuka misingi ya ubinadamu na pia kinaweza kuchochea mauaji dhidi yao.

Alisema katika jamii nyingi za Watanzania, wanaamini kuwa albino hawafi kifo cha kawaida bali hupotea, hali ambayo imekuwa ikichochea mauaji dhidi yao kwa baadhi ya watu kudhani kuwa viungo vyao si vya kawaida na vinaweza kusababisha utajiri.

Kwa msingi huo, alisema kitendo cha familia ya Witness kumzika mtoto wao ndani ya chumba cha biashara tena usiku wa manane pasipo kuishirikisha jamii, kinaweza kuchochea imani hiyo potofu kwamba albino hawafi bali hupotea.

“Albino ni binadamu kama binadamu wengine, tunazaliwa na kufa, hivyo mazishi yetu yanapaswa kufanyika hadharani kama vile mazishi ya watu wengine yanavyofanyika, lazima `wananzengo' (wanajamii) washiriki kwa taratibu zilizozoeleka ili kuondoa kabisa dhana potofu kwamba hatufi bali tunapotea,” alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa Tas Mkoa wa Mwanza, Mashaka Tuju, alisema kitendo kilichofanywa na familia ya Witness, kimewatia simanzi kiasi cha kuwafanya wawe na hisia mbaya dhidi ya familia hiyo.

Alifafanua kwamba ingawa Witness alikufa kifo cha kawaida baada ya kuugua kwa muda mfupi, lakini namna ambavyo mwili wake umezikwa ndiko kunakowatia shaka na kuhisi kuwa huenda kuna jambo limejificha.

Alisema kama lengo la familia hiyo lilikuwa kuepusha uwezekano wa watu wenye imani potofu kufukua kaburi la mtoto wao,  ni bora wangemzika katika makaburi ya jamii na kujengea zege lakini sio kumzika ndani ya chumba cha biashara tena kwa siri.

“Kutokana na mazingira ya tukio lenyewe, kama chama tumeamua kufungua jalada la shaka na kuiomba mahakama itoe kibali kwa Jeshi la Polisi kufukua kaburi la Witness ili tujiridhishe iwapo kweli mwili wake una viungo kamili kwa sababu hata mahali penyewe tulipoonyeshwa kuwa ndipo alipozikwa, hapaonyeshi dalili hizo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ernest Mangu, alisema hajapata taarifa.

Hata hivyo, alisema kama tukio hilo lipo ni vema viongozi wa Tas wakamuona Mkuu wa Polisi Wilaya ya Magu ili alishughulikie.

“Mimi sina taarifa pengine Tas walikuja ofisini wakati nimetoka, lakini nitafuatilia kujua kama walizungumza na wasaidizi wangu ili tumwelekeze OCD alishughulikie ingawa suala la kufukua kaburi linahitaji kwanza kibali cha mahakama,” alisema Kamanda Mangu.