Saturday, January 19, 2013

TANZIA



Aliyekuwa Ofisa Elimu (Taaluma) Wilayani Magu Mkoani Mwanza Ndugu Kamili Paul Dusu amefariki dunia.

Habari kuroka Wilayani Magu zinasema, Ofisa Elimu huyo kabla ya kukutwa na umauti, alikuwa kwenye kikao cha Kamati ya Elimu, Afya na Maji kilichokuwa kinafanyika Mjini Magu.

Kifo hicho kimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Magu, Bi Naomi Nnko na kusema kuwa, awali Ofisa Elimu Dusu alipokuwa kwenye kikao hicho alianguka ghafla, hali iliyomsababishia kufikwa na umauti baadaye.

Alisema kuwa baada ya kuanguka ukumbini, alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Magu, lakini hali yake ilikuwa mbaya zaidi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza ambako alipoteza maisha jana (18/01/2013) alfajiri.

Aidha, alisema kuwa, Ofisa Elimu huyo alikuwa akisumbuliwa na presha iliyokuwa inapanda na kushuka mara kwa mara.

Safu ya uongozi wa MDI, kwa niaba ya Wanamagu wote inawapa pole wale wote walioguswa na msiba huu popote pale walipo.

Bwana katoa na Bwana katwaa, jina lake lihimidiwe.
AMEN     

No comments:

Post a Comment