Mwenyekiti wa kijiji
cha Mwibiti kata ya Ikoma Mkoani Tabora anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kuiba Mahindi ya msaada yaliyotolewa na serikali kwa wananchi wa kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Suleimani Kumchaya ameeleza hayo alipokutana na waandishi
wa Habari Mkoani humo.
Amesema kuwa tuhuma
hiyo ya wizi wa mahindi, imetokea muda mfupi baada ya serikali kufikisha
mahindi kiasi cha Tani 17 wilayani humo kwa ajili ya kuwasaidia wananchi
wanaokabiriwa na njaa. Amewataja viongozi wanaoshiikiliwa kwa tuhuma hizo za
mahindi ya msaada kuwa ni Mwenyekiti wa Kijiji Hassan Ndimasalo, Katibu
Mtendaji Mathew Masiyu, Suleimani Nassib, Joahari Nassor, Johari Hamis, na John
Mhozya ambaye anaendelea kutafutwa.
Na Mdau wa MDI akiwa Tabora
No comments:
Post a Comment