Wednesday, April 17, 2013

Polisi Mwanza yawashikilia raia wawili wa Burundi

Mwanza.

Kutokana na kuenea kwa Dola Bandia za kimarekani katika maeneo mbalimbali nchini, Polisi MKoani Mwanza inawashilikilia raia wawili wa Burundi kwa tuhuma za kumiliki noti bandia za marekani 1100 zenye thamani ya pesa za kitanzania shilingi Milioni moja laki saba na themanini na mbili elfu.
Kukamatwa kwa raia hao wa Burundi kunafuatia polisi kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna watu wanamashaka nao.

Kamanda Mangu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ernest Mangu alisema raia hao wa Burundi walikamatwa maeneo ya uwanja wa ndege wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 684 ACR.
Kuhusu gari hilo kumilikiwa na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Kamanda Mangu, taarifa hizo wanazifanyia kazi, japo kuwa uhalifu hauna chama
Kamanda Mangu alitoa hadhari kwa wafanyabiashara mkoani Mwanza kutokana na dola bandia za marekani kuzagaa
Polisi inawatafuta watu wengine wakihusishwa kushirikiana na raia hao wa Burundi kutekeleza uhalifu.

No comments:

Post a Comment