Tuesday, April 30, 2013

TAARIFA YA MKUTANO WA MAGU DEVELOPMENT INITIATIVE (MDI) ULIOKETI TAREHE 20 APRILI, 2013 MERRYLAND MWENGE DAR ES SALAAM

AGENDA

1.UTAMBULISHO WA WANACHAMA WALIOHUDHURIA;
2.KUHUSU KUSAJILI UMOJA WANAMAGU;
3.MAREKEBISHO YA KATIBA KABLA YA KUSAJILI;
4.MENGINEYO;

Mwenyekiti alifungua kikao cha MDI mnamo saa kumi na moja na nusu baada ya sala ambayo iliongozwa na mjumbe mmoja.

UTAMBULISHO WA WANACHAMA WALIOHUDHURIA
Wanachama walijitambulisha kwa majina na mahali wanapoishi pamoja na chimbuko lao katika Wilaya ya Magu, walifanya hivi mmoja baada ya mwingine mpaka idadi yao ilipokamilika, yaani wanachama 26 ambao ndio kimsingi walihudhuria kikao. Pia Mwenyekiti alitoa taarifa kuwa kikao hicho kilikuwa na dhumuni kuu moja la kupata majina ya wanachama na saini zao kwa ajili ya kukamilisha usajili wa umoja wa Wanamagu.


KUHUSU KUSJILI UMOJA WA WANAMAGU
Mwenyekiti alianza kwa kutoa historia fupi ya Magu Development Initiative, kuwa ilianzishwa mwaka 2009 na malengo yake ya msingi ni kuwaweka pamoja wanamagu waishio Dar es Salaam na Wanamagu wote waliotawanyika kokote duniani ili kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na hatimaye kuleta maendeleo katika wilaya ya Magu.
Kutokea mwaka 2009 Umoja wa wanamagu haukuwahi kusajiliwa mpaka sasa ambapo kumekuwa na umuhimu mkubwa wa kuusajili ili kufanya kazi zake kisheria na kwa kuzingatia taratibu za nchi ya Tanzania kama sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGOs ACT No. 24 of 2002 inavyoelekeza.

MAREKEBISHO YAKATIBA KABLA YA KUSAJILI
Wajumbe walikubaliana kupitia Katiba ya Umoja kifungu kwa kifungu na kuipiisha baada ya marekebisho machache kama ifuatavyo;

Kiingilio na Michango kwa Mwezi
Kila mwanachama atatakiwa kulipa Tshs. 50,000 kama kiingilio. Kila mwanachama atatakiwa kutoa sh 7,000 kwa kila mwezi; Tshs. 5,000 kwa ajili ya kuimalisha umoja na Tshs. 2,000 kwa ajili ya shughuli za kijamii. Pia mwanachama atapoteza haki ya uanachama pale tu atakaposhindwa kulipa ada ya mwezi kwa miezi mitatu mfululizo au kukosa kuhudhuria vikao vitatu mfulurizo.


Nembo
Wanachama walikubaliana kuendelea na nembo iliyopo kuwa inatosha. Pia kutakuwa na mhuri ambao utakuwa na alama ya nembo ya MDI 


Utambulisho wa Jumuiya
Wanachama walikubaliana kuwa makao makuu ya jumuia yatakuwa Mwenge Dar es salaam, na ofisi nyingi zitafunguliwa katika mikoa yote ya Tanzania. Pia kulikuwa na makubaliano ya kugawa jiji la Dar es salaam katika kanda mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha wanachama kukutana kwa urahishi zaidi.

MAENGINEYO
1.       MSIBA
Kikao kilikubaliana kwamba mwanachama hai atapatiwa Tsh 200,000 kama atapatwa na msiba wa kufiwa na watu wafuatao;Baba , Mama, Mke au Mtoto.

2.       MATIBABU
Mwanachama atakayeugua na kuhitaji msaada wa kifedha kamati itampatia Tsh 100,000 kama mchango wa matibabu
Ajenda zingine zilihifadhiwa mpaka pale jumuia itaimalika nazo ni; ndoa, kukopeshana, kadi ya uanachama, uongozi wa kikanda

HITIMISHO
Baada ya kukubaliana kuyapitisha yaliyotajwa hapo juu, wajumbe walikubaliana kwa kauli moja kuwa, waiachie Kamati ya usajili ifanye kazi yake na itakuwa ikitoa taarifa kwa uongozi wa MDI mpaka usajili utakapokamilika.
Kikao kilifungwa kwa sala iliyoongozwa pia na mjumbe mmoja na Mwenyekiti alitoa kauli ya kufunga kikao kwa kusema kuwa, Mkutano mwingine utapangwa baada ya usajili kukamilika.

“Pamoja Tunajenga Magu yenye Maendeleo Endelevu”


No comments:

Post a Comment