Migiro Mkuu wa Chuo OUT
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania.
Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo,
Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.
Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu
wa 2013.
Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa
NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Dkt. Migiro
amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
30 Januari, 2013
No comments:
Post a Comment