AGENDA
1.
UTANGULIZI
2.
KUFUNGUA KIKAO
3.
KUKAMILISHA USAJILI WA UMOJA
4.
MAJUKUMU YA UMOJA KWASASA
5.
KUHAMASISHA MAWASILIANO BAINA YA WAJUMBE
6.
KUHIMIZA UTOAJI WA MICHANGO YA MWISHO WA
MWEZI
7.
MENGINEYO
8.
HITIMISHO
1. UTANGULIZI
Umoja wa Wanamagu ni umoja wa Hiari, usio wa
Kiserikali, usio wa Kisiasa wala wa kutengeza faida, wenye malengo ya jumla ya
kuwaweka pamoja wananchi wote wa Wilaya ya Magu iliyoko Mkoa wa Mwanza Tanzania
kwa dhumuni la Kuelemisha na Kuhamasisha wananchi kuendeleza Utamaduni na Tabia
ya kufanya Kazi kwa ushirikikiano unaojenga uwezo wa kujitegemea na kuleta
mabadiliko ya maisha bora kwa watu wote katika familia na jamii kwa ujumla ili
kujenga Amani,Umoja, Haki, Udugu, Demokrasia, Elimu, Uchumi, Utawala Bora, na Mazingira
Nadhifu katika Jamii.
2. KUFUNGUA KIKAO
Kikao kilifunguliwa na Mwenyekiti wa MDI
kuanzia saa Kumi na Nusu jioni, Maryland Pub, Mwenge Dar es salaam.
3. KUKAMILISHA USAJILI WA UMOJA
Ili M.D.I iweze kujiendesha kikamilifu
na kwa ufanisi ilihitajika kusajili umoja haraka iwezekanavyo ili kupata baraka
zote kutoka kwenye mamlaka husika ya nchi yetu ya Tanzania. Kwa hivyo kikao
kiliwateua wanachama watatu (3) wafuatao kushughulikia na kufuatilia usajili wa
MDI.
- Juma William Yabeja
- Samuel Magoiga
- Wilbert Maige
Wanachama hawa walipewa muda wa wiki
mbili (2) kuwasilisha taarifa ya usajili
huo.
Kuwa na umoja uliosajiliwa ni vizuri kwa
sababu zifuatazo;
KWANZA,umoja utakuwa na nguvu kisheria
ya kuweza kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo kama
tulivyojipangia kama Magu Development Initiative (MDI).
PILI, itatuwezesha kutekeleza majukumu
ya umoja ikiwa ni pamoja na kuweza kupata misaada ya wafadhili wa maendeleo ili
kusaidia katika kuteleza malengo ya umoja.
TATU, itatuwezesha kutimiza mahitaji ya
kikatiba kama yalivyoainishwa kwenye kaatiba ya MDI Ibara ya 9(10.2)
inayoelekeza jinsi ya kuwa na vyanzo mbadala vya mapato ya umoja.
NNE, kama jumuiya, tunatarajia kuwa na
mipango mikakati ya kukemea kwa nguvu zote dhana ya UCHAWI, Mauaji ya ALBINO,
Mauaji ya VIKONGWE, na mengineyo ambayo kwa muda mrefu yamechangia kudumaza
maendeleo ya wanaMagu na Magu kwa ujumla.
4. MAJUKUMU YA UMOJA KWASASA
Kama isemavyo elimu ndio ufunguo wa
maisha na wengi wetu ni mashaidi katika hili, kikao kilionelea kuwepo na
mkakati maalumu na endelevu kwa ajili ya kusomesha wanaMagu walio na mahitaji (wanaotoka
katika familia masikini). Kwa hiyo kutakuwa kunafanyika FUND RAISING kila mwaka
kwa ajiri ya kusomesha wanafunzi hao.
Zaidi tulishukuru Mwana Magu mmoja aitwaye
WILBERT MAIGE katika kikao hicho kwa kujitolea kusomesha mwanafunzi mmoja mwaka
huu (2013) kutoka shule ya sekondari ya kata ya SUKUMA. Kwa hili bado mlango
upo wazi kwa ajili ya mdau yeyote atakayeguswa kujitokeza kwa ajili ya kusaidia
wadogo zetu wapate elimu dunia.
5. KUHAMASISHA MAWASILIANO BAINA YA
WAJUMBE WA MDI
Pamoja na wajumbe wengi kujuana kupitia
facebook tu tulionelea kwamba umefika wakati mwafaka wa wanaM.D.I kuwa
tunakutana ktk vikao sehemu mbalimbali tulipo ili tuzidi kufahamiana zaidi kama
wanafamilia moja iitwayo (WANAMAGU). Tunaangalia uwezekano wa kupata kiongozi
kila Mkoa na Wilaya zetu kwa ajili ya kufanikisha jambo hili.
6. KUHIMIZA UTOAJI WA MICHANGO YA
MWISHO WA MWEZI
Kikao kilionelea kuendelea kuwaomba wajumbe
kujitokeza zaidi kwa ajili ya kutoa ada hii ambayo itatumika kujenga M.D.I na
sisi pia. Matumizi yake yatolewa kila hela itakapotumika kwa ajili ya shughuri
za M.D.I. Kiasi kilichobaki kitawekwa kwenye akaunti yetu No. 01J209830000 CRDB
BANK.
7. MENGINEYO
KWANZA, Kuweka
ajira zote zinazotolewa katika vyombo vya habari ndani ya M.D.I ili wadau
wapate kuziona na kuomba kazi hizo.
PILI, Kuwa na
ofisi kuu Dar Es salaam kama ilivyoainishwa kwenye Katiba.
8. HITIMISHO
Kama wanamagu na
wanachama wa umoja huu wa MDI, tuna jukumu la msingi la kushiriki katika
shughuli za kukuza umoja wetu na pia katika shughuli zake kwa kujitoa kwa dhati
kimaarifa, muda, kirasilimali na juhudi.
Nawatakia
kushiriki kwema kuijenga Magu Mpya.
MAENDELEO
YA MAGU…PAMOJA TUNAWEZA
No comments:
Post a Comment